Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Jeshi la Polisi, CP Nsatu Marijani amewathibitishia wananchi kuwa jeshi la polisi lipo imara kukabiliana na matukio ya uhalifu unaojitokeza na kusema kuwa kama kuna watu wana wasiwasi nalo basi wajaribu kufanya lolote.

”kama mtu ana wasiwasi na Jeshi letu basi ajaribu kufanya lolote maana wanasema asiyejua kufa basi akachungulie kaburi. Sisi tupo imara tutaendelea kuwa imara”.  Amesema Nsato

Ameongezea kuwa hali ya Usalama nchini imezidi kuimarika kwani hakuna tishio lolote la kiuhalifu linaloweza kutokea kwasababu Jeshi la Polisi limejipanga ipasavyo na halishindwi na chochote.

“Jeshi liko imara, matukio ya uhalifu nchini yamepungua sana, hakuna tishio lolote ambalo lipo nje ya uwezo wa Jeshi la Polisi kushindwa kulikabiri. Sisi kama Jeshi la Polisi tutaendelea kuhakikishia nchi hii inaendelea kuwa salama ili wawekezaji na wananchi waweze kufanya shughuli zao bila ya taflani yeyote”.

Nsato amesema hayo alipokuwa anatoa salamu za kumuwakilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro katika uzinduzi wa vituo vidogo vya polisi vinavyo hamishika ‘mobile Police Station’ ambapo vitaanza kutumika katika mkoa wa kipolisi Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema vituo hivyo vilivyo zinduliwa leo vitatumika kwa kadri ya maelekezo ya maeneo yenye uhalifu utakapotokea eneo fulani na endapo utapungua basi watavihamishia na kwenda eneo jingine lenye uhalifu.

Simba SC wabisha hodi Port Said Misri
Mourinho asisitiza De Gea kutokuondoka Old Trafford.