Baada ya tifutifu kubwa baina ya Rais wa nchi ya Kenya, Uhuru Kenyatta na mpinzani wake ambaye aliapishwa kama Rais wa watu, Raila Odinga, wawili hao wameamua kumaliza tofauti zao na kuahidi kufanya kazi pamoja, ambapo wamekubaliana kuunda mpango wa pamoja wa utekelezaji wa malengo ya pamoja
Makubaliano hayo yamefanyika katika ofisi za Raila Odinga, Jumba la Harambee Jijini Nairobi.
Ambapo Balozi, Martin Kimani ataongoza kuundwa kwa mpango huo upande wa Rais, Uhuru Kenyatta na mshauri wa Odinga Paul, Mwangi ndiye atakaye muwakilisha, kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotiwa saini na Kenyatta na Odinga.
Wawili hao wamethibitisha kuvunja uhasama uliopo baina yao mara baada ya kuhutubia, pindi walipotembelewa na Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani, Rex Tillerson ambaye alifanya ziara yake nchini humo.
Tillerson kwa muda mrefu amekuwa akiwataka wanasiasa hao kumaliza mzozo wa kisiasa uliopo kati yao.
-
Aliyesimamia Kuapishwa Raila amvaa, amuita msaliti
-
Japan yalalama uamuzi wa Trump juu ya ushuru
-
Waasi wafanya ubakaji wa halaiki, Jeshi la UN laongeza nguvu
Hivyo Raila na Kenyatta kwa nyakati tofauti walitoa hutuba na wote wakionekana kuwa na lengo moja la kuleta maendeleo nchini humo wakiamini kuwa maendeleo hayawezi kupatikana katika nchi zenye mizozo ya kisiasa.
“Maisha yetu ya baadaye hayawezi kupimwa kwa Uchaguzi Mkuu, bali utulivu wa nchi yetu na hali nzuri ya watu wetu, demokrasia ni mchakato ambao, hiari ya watu inasikilizwa lakini maslahi ya taifa lazima yatawale.” Amesma Uhuru Kenyatta
“Tukiendelea kuwa wabinafsi na waharibifu, hakuna kiwango chochote cha mageuzi ya kitaasisi ambacho kitaboresha maisha yetu.” amesema Raila Odinga.
Tumekubaliana tutaleta pamoja wananchi na kujadiliana kuhusu matatizo yanayoathiri taifa letu na wananchi, na kuunda taifa lenye umoja na lililo imara ambapo hakuna raia anayehisi ametengwa.
kenyatta amesema hayo na kumalizia kuwa, ”Huu ni mwanzo mpya kwa taifa letu. “Tunaweza kutofautiana lakini kusalia tukiwa tumeungana kama Wakenya.