Serikali ya Kenya imeviamuru vyombo vya habari kutopeperusha mubashara kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani (NASA) kama “Rais wa Wananchi” ambako kumepangwa kufanyika hii leo.

Kituo cha habari cha NTV kimesema kuwa serikali imeonya kuwa wale watakao tangaza sherehe hizo za kuapishwa ambazo ni kinyume cha sheria katika viwanja vya Uhuru Park vituo vyao vitafungiwa.

“Rais Uhuru Kenyatta na Makamu wake, William Ruto wamefanya mkutano wa pamoja na Waziri wa Usalama wa Ndani, Fred Matiang’i, Waziri wa Habari na Mawasiliano ya Kiteknolojia, Joe Mucheru na Mwanasheria Mkuu Githu Muigai kwa lengo la kuvitaka vyombo vya habari kutotangaza kuapishwa kwa Raila Odinga na Kalonzo Musyoka,” NTV imeripoti

Hata hivyo, Upinzani umesema utaendelea na sherehe hizo za kuapishwa huko eneo la Uhuru Park Jijini Nairobi pamoja na mamlaka husika kusema kuwa eneo hilo limefungwa kwa ajili ya kufanyiwa ukarabati.

 

 

Video: Mizinga ya nyuki yanaswa kwenye uwanja wa ‘kumuapisha’ Raila
Diamond ampokea Wema kikuza sauti na ‘I love you die’