Kesi ya kukutwa na viungo vya binadamu sehemu za siri za kike, imeshindwa kuanza kusikilizwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Dar es salaam Kisutu.

Kesi hiyo, inayomkabili mkazi wa Maswa mkoani Shinyanga, Salum Nkonja (23) imeshindwa kuanza kusikilizwa baada ya shahidi wa upande wa mashtaka kushindwa kufika Mahakamani.

Nkonja, anakabiliwa na mashtaka 11 yakiwemo ya kukutwa na viungo vya binadamu, zikiwemo sehemu za siri tano za kike na matiti, mafuvu mawili ya kichwa cha binadamu na nyara za Serikali. 

Awali, mtuhumiwa alifikishwa Mahakamani Juni 21, 2022 na kusomewa kesi ya uhujumu uchumi namba 32/2022 na wakili wa Serikali, Caroline Materu, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Ramadhani Rugemalira.

Mshtakiwa, anadaiwa kutenda makosa yake, Kati ya Oktoba 30, 2017 na Novemba 30, 2017 katika eneo la Ubungo lililopo Manispaa ya Ubungo na kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 2, 2022.

Mapigano jimbo la Blue Nile hali bado tete
Chiko Ushindi aachwa rasmi Young Africans, Sogne atafuata