Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi Jumatatu tarehe 6, Septemba 2021, inatarajiwa kutoa uamuzi wa pingamizi la mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi na Ugaidi.

Mbowe na wenzake wanapinga hati ya mashtaka yanayowakabili wakidai kuwa ina kasoro za kisheria na hivyo wanaiomba Mahakama hiyo iitupilie mbali.

Katika pingamizi hilo pamoja na mambo mengine wakidai kuwa Sheria ya Ugaidi ambayo wanashtakiwa nayo haijafafanua viambato vya kosa la Ugaidi na kwamba upande wa mashtaka haujazingatia masharti ya lazima ya sheria hiyo ambayo ni kueleza kusudio la vitendo vya ugaidi ambavyo washtakiwa wanatuhumiwa kuvitenda.

Gwajima: Msinyimane ujuzi
Tanzania, Ufaransa ni ujumbe wa utulivu na amani duniani