Kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake wawili, iliyopo katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, imeahirishwa hadi Septemba 3, 2021, kwa ajili ya upande wa mashtaka kuja kujibu pingamizi lililowasilishwa na washtakiwa.

Wakili wa Mbowe, Peter Kibatala amesema kuwa washtakiwa hao baada ya kufikishwa kwenye Mahakama hiyo, upande wa utetezi uliweka pingamizi kuhusu kesi kusikilizwa na Mahakama kuu ya Devision, ambapo Mahakama imetoa uamuzi leo kuwa inamamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Aidha Kibatala amesema wametoa hoja za kisheria kuwa washtakiwa wasisomewe mashtaka mpaka Mahakama ijiridhishe kama mashtaka hayo yamekidhi vigezo vya kisheria.

Mahakama hiyo imeamuru upande wa mashtaka kuja kujibu hoja za upande wa utetezi siku ya Ijumaa Septemba 3.

Tanzania, Canada kuendeleza uhusiano
Makusanyo ya tozo kujenga vituo vya afya 220