Klabu ya Singida Big Stars huenda ikamsajili Beki wa pembeni Nickson Kibabage ambaye ataondoka Mtibwa Sugar baada ya Dirisha Dogo kufunguliwa rasmi kesho Alhamis (Desemba 15).

Singida Big Stars imeonesha nia ya kumsajili Beki huyo ambaye aliwahi kucheza soka nchini Morocco akiwa na Klabu ya Difaâ El Jadidi, ikithibitika ataachana na Mtibwa Sugar aliyoitumikia tangu mwanzoni mwa msimu huu akitokea KMC FC.

Endapo mipango ya Klabu hiyo ya Singida itafanikiwa, Kibabae atakwenda kumpa changamoto Beki wa pembeni wa Singida Big Stars Yassin Mustafa, aliyesajiliwa klabuni hapo mwanzoni mwa msimu huu akitokea Young Africans.

Mapema leo Jumatano (Desemba 14) ujumbe wa Kibababe aliouandika katika Ukurasa wake wa Instagram ulisambaa kwa kasi, ukionesha ataondoka Mtibwa Sugar, baada ya kukamilika kwa Kandarasi yake.

Kibabage ameandika: Nipende kutoa shukrani zangu kwenu familia yangu ya muda wote @mtibwaofficial tumeanza na wakati mzuri kwenye huu msimu nawashukuru kwa upendo mlionionesha kijana wenu naimani tutakutana wakati mwengine tena mwenyezi mungu azidi kuwapa moyo huo huo UNITED WE STAND??❤❤

KMC FC, Coastal Union hapatoshi Uhuru Stadium
Kocha Vipers SC azitisha Simba SC, Horoya AC, Raja