Mabondia Nguli wa Tanzania, Selemen Kidunda na Tony Rashid, watapanda ulingoni Februari 24, katika pambano la kimataifa litakalofanyika kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza, jijini Dar es salaam.

Kidunda atapambana na Patrick Mukala wa DR Congo mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini, wakiwania ubingwa wa ‘ABU’ uzito wa Super Middle.

Wakati Tony atapambana kuutetea ubingwa wake wa ‘ABU’ uzito wa Super Bantam, dhidi ya Sabelo Ngebinyana kutoka Afrika Kusini.

Mbali na mapambano hayo mawili, kutakuwa na mapambano mengine makali ya utangulizi siku hiyo.
Promota wa pambano Hilo Saada Sakum kutoka KEMMON SPORTS AGENCY amesema mabondia wote tayari wamesaini na maandalizi ya pambano yanaenda vizuri kufikia sasa.

Kocha wa Singida Big Stars aitamani Simba SC
Ilamfya awashangaa wanaomshangaa