Profesa Harun Nyagori, ambaye ni Daktari binafsi wa marehemu Benard Membe amesema mwanasiasa huyo amefariki kwa kifo cha kawaida kilichotokana na maradhi ya kifua yaliyogusa mfumo wa hewa na kumsababisha matatizo ya kutopumua na kuitaja jamii kupuuza maneno kuwa membe ameuawa.
Prof. Nyagori ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na Wanahabari na kuongeza kuwa ameamua kutoa ufafanuzi huo baada ya kuenea maneno hasa mitandaoni Membe hajafa kifo cha kawaida, bali ameuawa kitu ambacho anakipinga kwani amekufa kifo cha kawaida ambacho kinaweza mpata yeyote.
Amesema, “na amekuwa mzima na amekuwa na afya ambayo imeimarika miaka yote, hajawahi kuwa na tatizo lolote sugu, amepata tatizo la ghafla la mfumo wa mapafu hewa, ambayo ikapelekea mgando wa damu kuwa nzito na kuzuia mapafu kupeleka Oxygen.”
Prof. Nyagori ameongeza kuwa, “kwa hiyo niondoe mkangamyiko ambao umekuwa ukizingumzwa huko mtaani, kwamba aidha Mheshimiwa Membe ameuawa, amepewa sumu, amepata matatizo mengine hiyo imani iondoke.
Enzi za uhai wake, Benard Membe amewahi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimaitaifa, katika Serikali ya awamu ya nne iliyokuwa chini ya Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.