Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Benard Kamilius Membe amefariki dunia muda mfupi uliopita katika Hospitali ya Kairuki iliyopo jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa za awali zinaeleza kuwa alipata changamoto ya kifua na kupelekwa alfajiri ya leo Mei 12, 2023 Hospitalini hapo na alifariki muda mfupi baadaye.

Bernard Kamilius Membe, alizaliwa November 9, 1953 na alikuwa mbunge wa jimbo la Mtama katika bunge la kitaifa la mwaka 2015 nchini Tanzania.

Mwaka 2016 alitaka kugombea urais kwa tiketi ya chama cha CCM, akashindwa kupata nafasi na mwaka 2019 Membe aliitwa mbele ya kamati kuu ya CCM na kuhojiwa kuhusu mashtaka ya kula njama dhidi ya rais na baadaye akafukuzwa katika chama kabla ya kurejeshwa tena.

Kwa taarifa zaidi usiache kufuatilia Dar24 Media.

Rage awaomba Simba SC kuishangilia Young Africans
TETESI: Mkataba wa Beleke kuvunjwa Simba SC