Mtuhumiwa Samson Petro ambaye aliwateka watoto wanne amefariki dunia kwa kupigwa risasi wakati akitaka kutoroka mikononi mwa Polisi jijini Arusha.

Mtuhumiwa alipigwa risasi mbili za miguu wakati akijaribu kutoroka na ndipo alipofariki dunia akiwa hospital ya Mount Meru.

Usiku wa tarehe 2 Septemba kijana mwenye umri wa miaka 18, Samson Petro alishikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuteka watoto katika mkoa wa Arusha na Geita.

Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo alithibitisha taarifa hizo za kukamatwa kwa mtekaji huyo.

Mwabulambo alisema kuwa kijana huyo alikamatwa katika nyumba ya kulala wageni ya Shitungului iliyopo mji mdogo wa Katoro akiwa na mtoto mdogo mwenye miaka miwili.

Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, ameeleza kuwa watoto wawili walipatikana huku watoto wengine wawili walikutwa wamefariki, ambapo mtuhumiwa apohojiwa alikiri kuhusika na mauaji hayo baada ya wazazi wa watoto kushindwa kupeleka fedha ambazo waliamriwa ili kuachia watoto hao.

MTuhumiwa aliwaua watoto wawili, Moureen David (6) na Ikram Salum (3) na kuwatumbukiza ndani ya shimo la maji taka.

 

 

Polisi matatani kwa kumtolea lugha chafu mwananchi
LIVE IKULU: Rais Magufuli akipokea ripoti ya uchunguzi wa Tanzanite na Almasi