Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Ester Bulaya ambaye pia ni Waziri Kivuli (Ofisi ya Waziri Mkuu) wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, amewataka Waziri, Jenista Mhagama na Mkurugenzi wa SSRA kujiuzulu, baada ya Rais Magufuli kuufuta mswada wa mabadiliko ya sheria ya utoaji mafao kwa wastaafu.

Bulaya ameandika katika ukurasa wake wa kijamii wa twitter ambapo amesema kuwa Waziri Mhagama na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii (SSRA) kufanya hivyo kwa kuwa wameshindwa kuwatetea wafanyakazi.

“Mh Jenista, na Mkurugenzi wa SSRA, mjiuzulu nimewashinda, hamkuwatetea wafanyakazi”, ameandika Bulaya.

Aidha, siku kadhaa baada ya habari hizo kuenea aliibuka Waziri Kivuli (Ofisi ya Waziri Mkuu) wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Esther Bulaya, ambaye alieleza kuwa kikokotoo hicho kinawaumiza wastaafu na hakikujulikana kwa wabunge.

Hata hivyo, wasimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii yaani Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii (SSRA), ilifafanua kuwa, lengo la kubaki kwa fedha hizo ni kumsaidia mstaafu kuishi vizuri kwa kuendelea kupata fedha ambazo zinasaidia maisha yake, kuliko kumpa zote ambazo huenda akazitapanya na kurudi katika umaskini.

 

Viongozi 9 wa upinzani watiwa mbaroni Sudan
Chris Brown aanza kupangua kesi ya nyani kukwepa jela