Bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka 2022/23 imepanda kutoka Shilingi 751.12 Bilioni hadi Shilingi 970.78 Bilioni mwaka 2023/24 sawa na ongezeko la asilimia 29.24 ambapo katika mwaka 2021/22 ilikuwa ni Shilingi 294.16 bilioni.

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ameyasema hayo hii leo Mei 8, 2023 wakati akiomba kuidhinishiwa fedha hizo na Bunge na kuongeza kuwa, kati ya fedha hizo, Shilingi 767.83 Bilioni ni fedha za maendeleo.

Amesema, mwaka 2022/2023 fedha zilizoidhinishwa ni Shilingi 751.12 Bilioni ambapo fedha za maendeleo zilikuwa Shilingi 569.97 Bilioni na hivyo ongezeko hilo ni Shilingi 197.86 Bilioni ambazo ni fedha za maendeleo na siyo matumizi ya kawaida.

Bashe ameongeza kuwa, “Fedha hizo zimetengwa kwa ajili ya kuimarisha utafiti wa kilimo, uzalishaji wa mbegu, utoaji wa ruzuku, kilimo cha umwagiliaji, miundombinu ya uhifadhi wa mazao, kuimarisha huduma za ugani, upatikanaji wa masoko ya mazao na kuendeleza programu ya Jenga Kesho iliyo bora.”

Kocha Julio matumaini kibao Ligi Kuu
Mkama aridhishwa kasi ujenzi Ofisi ya Makamu wa Rais