Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara, Wilaya ya Masasi linamshikilia mkazi wa kijiji cha Mkwapa, Sandali Omari(40) kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa la pili anayesoma shule ya msingi Mkwapa, baada ya kumdanganya kumpa kilo Moja ya korosho.
Tukio hilo limetokea novemba 17 mwaka huu ambapo siku ya tukio mwanafunzi huyo aliondoka nyumbani kwao akiwa na wenzake na kwenda kwenye sherehe ya unyago katika nyumba ya jirani ambako lilikuwa linapigwa disko la kunogesha sherehe, ambako ndiko alikutana na mtu huyo.
Aidha, mtendaji wa kijiji cha Mkwapa, Mohamedi Dadi amesema kuwa baada ya mtuhumiwa kufanikiwa kumdanganya mwanafunzi huyo kwa kumpa kilo ya korosho ili imsaidie mahitaji ya shule, ambayo kwa sasa ni sh.3,300. walipofika chumbani kwake alimtishia kitu chenye ncha kali na hatimaye kumbaka.
Amesema kuwa mtuhumiwa alikamatwa baada ya kufuatiliwa na watu waliokuwa naye kwenye sherehe, kisha wakamuita Mwalimu Mkuu na Mgambo ambao walifanikiwa kumkamata usiku huo na kumfungia katika ofisi ya kijiji na asubuhi akapelekwa kituo cha polisi wilaya ya Masasi ambako anashikiliwa hadi sasa.
-
Mchungaji Komando Mashimo amdhamini Amber Rutty
-
Majaliwa aagiza kukamilika kwa wakati mradi wa maji Chato
-
Kawafundishe uzalendo unao waongoza, vinginevyo wataishia Gerezani- JPM
Kwa upande wake Baba mzazi wa mwanafunzi huyo amesema kuwa mtoto wake bado ni mdogo sana kufanyiwa kitendo cha kinyama.