Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un ametangaza hali ya dharura na kuufunga (lock-down) mji ulio mpakani, baada ya mtu aliyebainika kuwa na dalili za virusi vya corona kurudishwa nchini Korea Kusini, alipojaribu kuvuka mpaka.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Korea Kaskazini (KCNA), Kim Jong Un alifanya kikao cha dharura kujadili hali hiyo, kwakuwa hadi sasa hakuna kisa chochote cha corona kilichothibitishwa nchini humo.
Mtu huyo aliyekutwa na dalili za virusi vya corona, anadaiwa kuwa alitaka kupita mpakani mwezi huu bila kufuata taratibu, na ni mmoja kati ya watu waliokimbia nchi hiyo na kukimbilia Korea Kusini.
“Tukio hilo la dharura limetokea katika mji wa Kaesong ambapo mtu huyo aliyeikimbia Korea Kaskazini miaka mitatu iliyopita, alibainika kuwa na dalili za virusi vya corona na alirudishwa Julai 19, 2020, akijaribu kuvuka mpaka bila kufuata taratibu za kisheria,” KCNA imeripoti.
Korea Kaskazini inakabiliwa na vikwazo mbalimbali vya kiuchumi vya Umoja wa Mataifa. Hivyo, endapo itakabiliwa pia na maambukizi ya virusi vya corona huenda ikawa katika hali mbaya zaidi.
Mlinzi wa Mkapa asimulia maisha yake ndani ya Ikulu, alivyojenga msikiti