Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Kim Poulsen ametangaza kikosi cha timu hiyo kuelekea mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2022, dhidi ya DR Congo utakaochezwa mwezi Septemba.
Taifa Stars itaingia kambini Agosti 24, jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo huo utakaoambatana na ule dhidi ya Madagascar.
Wachezaji walioitwa kambini tayari kwa maandalizi, upande wa Walinda Lango yupo Aishi Manula [Simba], Metacha Mnata, Ramadhani Kabwili [Yanga], Wilbol Maseke [Azam FC].
Mabeki: Shomari Kapombe [Simba], Israel Mwenda [Simba], Erasto Nyoni [Simba], Dickson Job [Yanga], Bakari Mwamnyeto [Yanga], Kennedy Juma [Simba], Lusajo Mwaikenda [Azam FC], Abdulrazack Mohamed [Azam FC], Mohamed Hussein [Simba], Nickson Kibabage [Youssoufla FC-Morocco], Edward Manyama [Azam FC]
Viungo: Ayoub Lyanga [Azam FC], Meshack Mwamita [Gwambina FC], Novat Dismas [Maccabi Tel Aviv-Israel], Mzamiru Yassin [Simba], Mudathir Yahya [Azam FC], Feisal Salum [Yanga], Salum Abubakar [Azam FC], Zawadi Mauya [Yanga].
Washambuliaji: Iddy Selemani [Azam FC], Abdul Hamis Seleman [Coastal Union], Mbwana Samatta [Fenerbahce-Uturuki], John Bocco [Simba] na Simon Msuva [Wydad Athletic-Morocco]