Aliyekuwa Kiongozi wa kundi la Mungiki, Maina Njenga amefikishwa katika Mahakama ya Nakuru kusomewa mashtaka ya kuwa mwanachama wa kundi haramu na kujihusisha na vitendo vya uhalifu uliopangwa.
Maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai -DCI, nchini Kenya wamekuwa wakimwinda Njenga baada ya bastola mbili na misokoto ya bangi kupatikana katika makazi yanayodaiwa kuwa yake katika eneo la Wanyororo jijini Nakuru.
Katika operesheni hiyo, Maafisa hao pia walikamata watu wanane na hapo awali walisema “Njenga anatafutwa ili ahojiwe baada ya bangi na bunduki kupatikana katika boma linalodaiwa kuwa lake.”
Aidha, Maafisa hao kupitia taarifa iliyochapisha kwa ukurasa wa mtandao wa Twitter walitaka aliye na habari za wapi aliko kiongozi huyo wa zamani wa Mungiki, ambaye tayari yuko mafichoni, aziwasilishe kwa DCI.
Hata hivyo, Njenga alionekana kwenye mazishi ya Mama Mukami Kimathi ambaye hadi kifo chake alikuwa mjane wa mpiganiaji uhuru Shujaa Dedan Kimathi na alikataa baadaye.