Uongozi wa Dodoma Jiji FC, umeweka wazi kuwa nyota wao wawili ambao walikuwa wameumia, Collins Opare na Stephen Sey, wameanza kurejea kwenye uimara jambo linalowapa matumaini ya kuwa nao mechi zilizobaki.

Afisa Habari wa Dodoma Jiji Moses Mpunga amesema maandalizi kwa mechi mbili zilizobaki yapo vizuri na wachezaji wao ambao walikuwa nje kwa muda wameanza kurejea kwenye uimara.

“Tunamshukuru Mungu maandalizi yanaendelea vizuri na wachezaji wapo imara ikiwa ni pamoja na Stephen Sey ambaye alikuwa nje kwa muda baada ya kuumia.

“Collins Opare yeye pia alipata maumivu kwenye mechi ya kirafiki, lakini kwa sasa anaendelea vizuri, tunaamini kwenye mechi zijazo benchi la ufundi likiona ni vema litawatumia wachezaji wetu,” amesema

Young Africans yajiamini kimataifa
Robertinho kukabidhi faili la atakaowasajili