Mahakama ya hakimu mkazi ya Lusaka nchini Zambia imeamuru kuwa kiongozi wa chama cha upinzani cha United Party for National Development (UPND), Hakainde Hichilema afikishwe katika Mahakama Kuu ya nchi hiyo kwa kosa la uhaini.

Taarifa za kinachoendelea katika mahakama hiyo zimekuwa zikitolewa na chama chake kupitia mtandao wa twitter na kupitia akaunti ya mwanasiasa huyo.

Hichilema na wenzake watano wamefunguliwa mashtaka ya uhaini baada ya msafara wake kudaiwa kuingilia msafara wa rais wa nchi hiyo, Edgar Lungu mwezi Aprili mwaka huu.

Hata hivyo, wanasheria wa mwanasiasa huyo wamekuwa wakipinga mashtaka hayo dhidi ya mteja wao na kuhoji mamlaka ya afisa aliyefungua mashtaka hayo.

Kabla ya kukamatwa, kiongozi huyo wa upinzani alifukuzwa kutoka kwenye makazi yake jijini Lusaka.

 

Video: Dkt. Mpango aondoa ushuru kusafirisha mazao yasiyozidi tani 1
Timu ya mpira wa kikapu Dar kushiriki mashindano Kenya