Timu ya mpira wa kikapu ya mkoa ya Dar es salaam inatarajia kuondoka Ijumaa Juni 9, 2017 kuelekea kwenye mashindano ya miji nchini Kenya, ambapo timu 6 kutoka katika miji mikubwa ya Afrika Mashariki zitashiriki.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Mkurugenzi wa mawasiliano wa Ligi ya mpira wa kikapu Dar es salaam (RBA), Peter Mpangala amesema kuwa timu hiyo itashiriki mashindano hayo yatakayofanyika Nairobi, nchini Kenya na miji ambayo itashiriki ni Nairobi, Mogadishu, Kigali, Juba na Dar es salaam.

Amesema mashindano hayo yataanza Juni 11, 2017 na michuano hiyo inatarajiwa kuonekana moja kwa moja kwenye runinga.

Kiongozi wa upinzania Zambia kizimbani kwa uhaini
?Live: Yanayojiri Bungeni Serikali ikiwasilisha wa Bajeti Kuu 2017/2018