Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO limesema lilirekodi visa 470,000 viliripotiwa mwaka wa 2022, ikiwa ni ongezeko kubwa kuwahi kutokea, ikilinganishwa na visa 220,000 vya mwaka 2021, huku likitoa rai kwa Mataifa kudhibiti Ugonjwa huo.
Kupitia tarifa yao, Wataalam wa WHO wanaamini kuwa takwimu hizo bado hazijitoshelezi na katika makadirio ya awali, lilitabiri kuwepo wagonjwa milioni 1.3 hadi 4 na uwepo wa vifo hadi watu 143,000 kwa kila mwaka.
Aidha, wamezitaja nchi za Afghanistan, Cameroon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Malawi, Nigeria, Somalia na Syria kuwa ziliathirika zaidi katika mwaka ambao mlipuko huo ulikuwa ni wa juu zaidi.
Hata hivyo, milipuko ya Ugonjwa wa Kipindupindu inahusishwa zaidi na uhaba wa maji ya kunywa mahitaji, umaskini na migogoro, ambapo kadri milipuko inavyoongezeka, ndivyo ugumu wa kudhibiti inavyozidi kuwa mgumu.