Shirika la madaktari wasio na mipaka – MSF, nchini Kenya limeonya uwezekano wa dharura ya afya katika kambi kubwa ya wakimbizi nchini humo Daadab ,kufuatia mlipuko wa Kipindupindu ambao umeambukiza watu 1120 tangu Novemba mwaka uliopita na kusababisha vifo vya watu wawili.

MSF imetoa wito kwa mashirika ya misaada kuingilia kati, ikieleza kuwa msongamano mkubwa wa wakimbizi umesababisha uhaba wa maji na vyoo, hali ambayo inafanya kuwa vigumu kudhibiti msambao wa Kipindupindu.

Mkuu wa MSF Ukanda wa Kenya, Hassan Maiyaki amesema hali hii haijawahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita huku akiongeza kuwa, “ukubwa wa hali hii inahitaji msaada dharura ,haswa usambazaji wa maji na udumishaji usafi.”

Aidha, MSF imeitaka serikali ya Kenya kuharakisha mchakato wa kufungua kambi ya nne ya Ifo 2 ili kupokea wakimbizi wanaoendelea kuwasili na kupunguza mzigo wa kugawa raslimali.

Dadaab iliyo na kambi zingine tatu, Daghaley Ifo na Hagadera, ina wakimbizi zaidi ya wakimbizi 300,000 na idadi hiyo imekuwa ikiongezeka kutokana na ukame ulioshuhudiwa nchini Somalia.

Stephane Aziz Ki aomba radhi Young Africans
Aishi Manula kuigharimu Simba SC, Taifa Stars