Wakati Mlinda Lango wa Simba SC Aishi Manula akienda Afrika Kusini kufanyiwa matibabu ya majeraha ya nyonga, huenda mchezaji huyu akawa nje ya uwanja kwa muda usiopungua miezi mitatu jambo linaloweza kuipa wakati mgumu Simba na timu ya Taifa ‘Taifa Stars’.

Kukosekana kwa Manula ni pigo kwa klabu hiyo kutokana na ratiba ya Simba SC msimu ujao kwenye mashindano inayoshiriki, lakini vilevile hadi Taifa Stars itakayocheza mechi ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Niger, Juni 18 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam.

Manula aliumia nyonga na kumfanya akose mechi za Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika pamoja na Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ na mechi zote za Ligi Kuu zilizosalia.

Kukosekana kwa Mlinda Lango huyo kunafanya pengo lake kuwa kwenye wakati mgumu kuzibwa kwani makipa ambao alikuwa anaitwa nao Taifa Stars ni Beno Kakolanya na Metacha Mnata ambao wote hawajawa wakitumika mara kwa mara katika timu wanazochezea.

Manula pia atakosa mechi za mashindano mapya ya Shirikisho la Soka Afrika yanayoitwa Afrika CAF Super League ambayo Simba SC itashiriki ikitarajiwa kuanza Agosti 2023 mwezi ambao mchezaji huyo atakuwa ndio amepona majeraha ambapo baada ya hapo atahitaji muda wa kuwa fiti ili arejee uwanjani.

Hilo linailazimisha Simba SC kuingia sokoni kusaka kipa mpya kwani itabaki na Ally Salim kutokana na kuondoka kwa Kakolanya baada ya msimu kumalizika.

Na inaripotiwa viongozi wa Simba SC wameanza mchakato wa kutafuta kipa mwingine mwenye uzoefu na kiwango kama Manula ili alete ushindani kikosi kwenye chao.

Akizungumzia hali na mazingira ya matibabu ya Manula Daktari wa zamani Young Africans, Shecky Mngazija amesema tatizo la nyonga hupona kwa upasuaji mkubwa au mdogo kulingana na mgonjwa alivyo.

Dk Mngazija amesema upasuaji mdogo huwa hauchukui muda mrefu kupona ila mkubwa unachukua muda mrefu.

“Kupona kwa haraka muda mwingine (inategemea na) umri wa mchezaji mwenyewe. Akiwa mkubwa unachelewa na akiwa mdogo atawahi tu ni kawaida.

“Kitukingine ni usahihiwamatibabu. Akipata matibabu mazuri kwa namna moja ama nyingine atawahi kupona lakini kingine ni lishe nzuri ambayo anaipata mgonjwa mwenyewe.”

Tabibu huyo wa matatizo ya kiafya kwa wanamichezo aliongeza kuwa: “Ukiwa umetoka kufanyiwa upasuaji inabidi uachane na kula vyakula vyenye protini nyingi na badala yake uangazie zaidi kwenye upande wa vyakula vyenye calcium (madini chuma), lakini pia unatakiwa ujitunze ukiambiwa utembelee magongo mawili inabidi ufanye hivyo na kuepuka magonjwa nyemelezi.”

MSF yaonya mlipuko wa Kipindupindu, 1120 waathiriwa
Bei ya Mafuta nchini kuporomoka zaidi - Makamba