Katika sehemu ya kwanza la makala hii tuliona kuwa Bara la Afrika linajulikana ulimwenguni kwa sifa nyingi ikiwemo utajiri wa rasilimali, umaskini, ukosefu wa usalama na ufisadi na sehemu hiyo ya kwanza tulimuangalia muasisi wa Taifa la Afrika ya Kusini, Hayati Nelson Mandela.

Baadaye katika sehemu ya pili tukamuona Mkongwe Haile Selassie, mtawala wa Ethiopia kuanzia 1916 hadi 1974, kisha sehemu ya tatu moja tukamuona Kwame Nkrumah, Rais wa kwanza mzawa wa Ghana na mwanzilishi wa Taifa la Ghana, akiwa ni mwana-Pan-Africanist ambaye alianzisha Umoja wa Afrika – AU, ambao zamani ulijulikana kama Umoja wa Umoja wa Afrika – OAU.

Aidha, tuliona jinsi ambavyo hakuridhika na uhuru wa nchi yake pekee, akisema uhuru wa Ghana hautakuwa na maana kama nchi zingine za Kiafrika zitaendelea kuwa chini ya Utawala wa Kikoloni na hii ikaoneonesha jinsi mwanaharakati huyu alivyokuwa tayari kujitoa muhanga kwa ukombozi wa Bara zima la Afrika.

“Matendo bila mawazo ni bure. Mawazo bila matendo ni upofu.” Dkt. Kwame Nkurumah.

Uchaguzi wa kwanza wa Ghana mwaka 1951, Nkurumah aligombea akiwa jela, chama chake CPP, kilipata viti 34 kati ya viti 38 vya Baraza la Kutunga Sheria (LEGCO) na GCP cha Danquah kiliambulia viti vinne na Nkrumah mwenyewe katika Jimbo la Accra alipata kura 20,780 kati ya kura 23,122 zilizopigwa; mpinzani wake kutoka GCP alipata kura 2,342.

Habari za ushindi huo zilimfikia Nkrumah akiwa jela Februari 12, 1951; naye Gavana wa nchi hiyo, Aden Clarke, akalazimika kumtoa kifungoni siku hiyo na kumwomba aunde Serikali ya Mpito. na ilipofika Julai 1953, huku akionesha dhahiri kupoteza subira, Nkrumah alishinikiza kuundwa kwa Serikali yenye madaraka kamili “bila kuchelewa.”

Hata hivyo, ulizuka mtafaruku kati ya Nkrumah aliyetaka kujenga Taifa huru la kidemokrasia na la kisiasa, na Watawala wa kijadi (Machifu) waliotaka kubakia na madaraka yao ya wakati wa mkoloni, ghasia na machafuko yakazuka na nyumba ya Nkrumah ikashambuliwa kwa mabomu.

“Ikiwa tutawatambua kwa matunda yao, lazima kwanza wazae matunda.” Dkt. Kwame Nkurumah.

Kwa kisingizio cha kutaka kupata matakwa sahihi ya wananchi, Serikali iliagiza ufanyike uchaguzi mwingine na licha ya ushindi mkubwa kwa mara ya pili kwenye uchaguzi wa mwaka 1954 kuelekea uhuru kamili, Serikali ya Uingereza ilikataa kutamka tarehe ya uhuru na badala yake ikatangaza uchaguzi mwingine kufanyika mwaka 1956.

Katika uchaguzi huo, CCP kilipata kura 398,000 dhidi ya kura 299,000 za upinzani; na kwa viti vya LEGCO, kilipata viti 72 kati ya viti 104. Kwa matokeo hayo, Uingereza ikaridhia Ghana kupata uhuru Machi 6, 1957.

Mwandishi wa Kimarekani, John Gunther aliyekutana na Nkrumah siku ya uhuru anaelezea haiba ya kiongozi huyo katika Kitabu chake “Inside Africa”, ifuatavyo: “Mwendo, mwenendo na hisia (gesture) zake ni zenye mvuto, nguvu na utulivu wa kuhuisha; hana mikogo wala kauli tata za kutia chumvi”.

Eneo la Makumbusho ya Dkt. Kwame Nkurumah nchini Ghana. Picha ya 123RF.

Nkrumah, akiwa bado kapera hadi Desemba 1957, maisha yake yalitawaliwa na siasa pekee kuliko vitu vingine, hakuwa mpenzi wa michezo, kinywaji, sigara wala starehe za aina yoyote na alikuwa mtu mpweke, mwenye fikra wa kuwaza na kuwazua nyakati zote na hakuamini wenzake na kwa nadra alitaka ushauri wao.

Aliweza kuchanganyika na wanawake kwa urahisi lakini hakupenda kuhusiana nao kwa karibu, iwe kwa upendeleo maalum wa kivikundi au mmoja mmoja hivi kwamba kabla ya uhuru aliwahi kusema hakuwa na muda wa kuoa, hadi aliposhinikizwa na mfumo wa Serikali baada ya uhuru.

Bila kumjulisha mtu, lakini kwa shingo upande, na pengine kwa kushauriwa na aliyekuwa Rais wa Misri, Gamal Abdel Nasser, Nkrumah aliamua kuoa mke kutoka Misri, mwanamke ambaye hakuwahi kumsikia wala kukutana naye kabla ya hapo hadi siku alipoletwa Ghana siku ya kufunga ndoa, Desemba 30, 1957, iliyoshuhudiwa na watu wasiozidi 30.

“Nguvu zinazotuunganisha ni za asili na ni kubwa zaidi kuliko mvuto uliowekwa juu ambao hutuweka kando.” Dkt. Kwame Nkurumah.

Binti huyo wa Kimisri, Fathia Rizk, aliongea lugha ya Kiarabu pekee, na kidogo sana, Kifaransa kwa kubabia; wakati Nkrumah aliongea Kiingereza kufanya wanandoa hao kuhitaji wakalimani. Kwa nini Nkrumah alichagua ndoa baridi kama hiyo?

Erica Powell, mwanamama wa Kiingereza Msaidizi maalum wa Nkrumah, aliyeachiwa na Wakoloni kumsaidia kuweka sawa mambo ya utumishi na utawala (kama ambavyo tu Mwalimu Nyerere alivyopewa Mama Joan Wickens mwaka 1961) wakati wakiondoka.

Anamnukuu Nkrumah katika kitabu chake “Private Female Secretary in the Gold Coast”, akimwambia: “Erica, Je, wajua kwamba mimi ni mtu mpweke nisiye na rafiki wala makundi, na kwamba kwangu kilichomhimu ni Kazi tu?”

Dkt. Kwame Nkrumah akiwa na mkewe Fathia Nkrumah. Picha ya Popperfoto/Getty Images

Aliwahi kumwambia (1965) pia kwamba, kitu ambacho angependa kufanya ni kujiuzulu Urais na kutumia muda wake wote kwa shughuli za Umoja wa Afrika.

Erica anakiri Nkrumah aliwahi kumtamkia pia kuwa, ikitokea kwamba ameoa, kwake suala la mke, watoto na mambo ya kifamilia kwa ujumla yasingekuwa masuala ya Kiserikali bali ya kibinafsi, akisema “ni hatari sana, na kwa kweli ni ubatili mtupu, kwa mke na familia kujiona kuwa sehemu ya utawala na Serikali”.

Nkrumah alimwambia Erica, ndoa haikumuondolea upweke, akasema: “Wajua Erica; sikutaka kuoa, wala sikuoa kwa kupenda ila kwa sababu ya Urais”.

Dkt. Kwame Nkurumah akiwa na Malkia Elizabeth. Picha ya Ghana State.

Erica hakuelewa, kwa nini mtu wa hadhi kubwa kama Nkrumah, mwenye elimu, akili na busara kubwa, aliamua kuoa msichana mdogo na ambaye hawakuelewana kwa kizuizi cha lugha. Hapa kulikuwa na mshabihiano uliofichika.

Ilitokea kwamba, Nkrumah alioa Misri si kwa bahati mbaya, kwa Rais mwanaharakati Kanali Nasser, mwenye siasa za mrengo wa Kikomunisti, aliyeingia madarakani kwa kupindua kijeshi Serikali ya Mfalme Farouk mwaka 1956.

Nasser na Nkrumah, licha ya kuwa miongoni mwa waasisi wa OAU, walikuwa Waasisi pia wa Umoja wa Nchi zisizofungamana na upande wowote duniani (Non-aligned Movement – NAM), pamoja na Josef Bronz Tito (Yugoslavia) na Pandit Jawaharl Nethru (India).

Makala: Mfahamu Rais mteule wa Nigeria, aliyekwepa kuingia jela akaingia Ikulu

Aliyekuwa Rais wa Ghana John Dramani Mahama akihojiwa na vyombo vya Habari mbele ya sanamu ya Dkt. Kwame Nkurumah. Picha ya TV3.

Wanne hao walikuwa pia wanamstari wa mbele wa kwanza na majabali dhidi ya ukoloni mkongwe, ukoloni mamboleo na ubeberu wa kimataifa.

Lakini pengine sababu kubwa zaidi kwa Nkrumah kumuoa binti huyo wa Kiarabu, ilikuwa ni kujaribu kuimarisha mshikamano wa Kiafrika (Pan-Africanism) kwa kujenga tafsiri mpya kwamba “Mwafrika” maana yake si “Mtu mweusi” pekee, bali ni “mzalendo yeyote mkazi wa Afrika mwenye mapenzi mema kwa Afrika”.

Mafanikio ya Nkrumah kisiasa hayakuwa bila mikwara kama anavyoelezea Genevova Marais, katika kitabu chake “Kwame Nkrumah As I knew Him” kwamba, “Kadri alivyopata mafanikio nchini, ndivyo alivyozidi kutowamini marafiki zake wa karibu, bila kujali jinsi walivyojitahidi kuonesha utii kwake.

Moja ya kumbukumbu za kumuenzi Dkt. Kwame Nkurumah nchini Ghana. Picha ya KNUST.

Kwa jinsi hii, alipoteza ushirikiano kiserikali na kubakia kuungwa mkono na Wana-CCP pekee, waliomwambia kile tu waliona angefurahi kusikia na kuacha mambo mengine yajiendee hovyo hivyo”. Kwanini?

Erica Powell anasema, tatizo la Nkrumah, na la madikteta wema wote (benevolent dictators) ni kwamba, “alikuwa hatabiriki; kwa haiba, aliweza kubadilika ghafla, akawa mkali kupindukia, asiyeambilika; lakini alikuwa mcheshi pia na mwenye kufikiria upya jambo akiona inafaa kufanya hivyo”.

Nkrumah alipinduliwa na Jeshi lake Februari 24, 1966 akiwa mjini Beijing, China akielekea Hanoi, Vietnam kama Kiongozi wa Kimataifa mwenye jukumu la kusuluhisha vita ya Vietnam, kati ya Vietnam na Marekani enzi hizo za vita baridi. Alirejea Afrika lakini si Ghana, bali kama mkimbizi uhamishoni nchini Guinea.

Mtoto wa Mfalme Philip, Duke wa Edinburgh, akiwa ameketi na Waziri Mkuu wa Ghana Dkt. Kwame Nkrumah, wakati wa tafrija ya kiraia. Picha ya AP.

Mwalimu Nyerere alitaja sababu zenye ukakasi kidogo, juu ya kuangushwa kwa Nkrumah kuwa, “alifanya kosa kuruhusu rushwa na rushwa ikamlemea”. Je, ilikuwa rushwa pekee iliyomwondoa?
Kuanguka kwa Nkrumah hakukuja kwa sababu ya kukithiri kwa rushwa nchini Ghana, la hasha, wala si kwa sababu ya uongozi mbaya au kuharibika kwa uchumi.

Nkrumah aliangushwa kwa kuthubutu kuchokoza ubeberu wa Kimataifa na kwa kutaka kuunganisha Afrika na nchi za dunia ya tatu kupambana na ubeberu huo.

Ndoto ya Nkrumah ya kuunda Shirikisho la Mataifa ya Afrika (United States of Africa) – “USA” mithili ya USA ya Marekani; kuunda ngome ya Kijeshi Afrika, mithili ya Umoja wa Kujihami Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) na kwa kujaribu kuinasua Afrika kutoka kwenye ushawishi wa Mataifa makubwa (Non-alignment) ilichangia pia.

Kwame Nkrumah akipokea nukuu, Julai 1958 katika Chuo Kikuu cha Lincoln. Picha ya Pen Libraries.

Dalili zilijionesha mapema. Kuchapisha kwake kitabu, “Neo-Colonialism: The Highest stage of Imperialism” (Ukoloni Mamboleo: Hatua ya Juu kabisa ya Ubeberu) Oktoba 1965 kushambulia Ubeberu, kuliitia kichaa Marekani na kufuta msaada wa dola milioni 35 kwa Ghana.

Miezi minne baadaye, akapinduliwa kwa msaada wa Shirika la Kijasusi la Marekani (CIA).
Kanali A.A Afrifa aliyeongoza mapinduzi hayo, alielezea sababu hizo miezi mitano baadaye, katika kitabu chake “The Ghana Coup”, kuwa ni “ndoto za Nkrumah juu ya Pan-Africanism na Muungano wa Afrika; kuunga mkono ukombozi wa kitaifa nchini Kongo na kwingineko, na chuki bila sababu dhidi ya nchi rafiki zetu za Kimagharibi.”

Ni ukweli usiopingika, wala si uzushi, kwamba kupinduliwa kwa Nkrumah ulikuwa ushindi kwa ubeberu wa Kimataifa na ukoloni mamboleo Afrika na kuanzia hapo, msukumo wa Afrika kuungana umetoweka, udikteta na uporaji wa rasimali za Afrika umetia fora, Afrika inazidi kudhoofika katika nyanja zote kuliko mwanzo, haina jeshi la pamoja la kujilinda wala kutetea uhuru wake ila kwa “msaada” kutoka nje, Afrika iko njia panda.

Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Kushoto), akifurahia jambo na Rais wa kwanza wa Ghana, Dkt. Kwame Nkurumah. Picha ya LSE.

HUYU NDIYE KWAME NKRUMAH JABALI LA UKOMBOZI WA AFRIKA, “Kwa mamilioni ya watu ndani na nje ya Afrika, Kwame Nkrumah ndiye Afrika na Afrika ndiyo Kwame Nkrumah, kwa Wakoloni na Mabeberu jina la Nkrumah ni laana kwao, kwa Masetla na Walowezi jina lake ni onyo kwamba siku zao zinahesabika, kwa Waafrika wanaokandamizwa kwa ukoloni na ubeberu wa kimataifa, jina lake ni pumzi ya matumaini, nyenzo ya uhuru, ushindi, udugu na usawa kwa wote”.

Ndivyo yalivyosomeka maneno ya bango moja mjini Accra, Ghana miaka ya 1960 wakati wa kilele cha harakati za Uhuru barani Afrika. Ghana ilipata uhuru Machi 6, 1957 chini ya Dakta Kwame Nkrumah kama Rais wa kwanza.

Lakini Nkrumah hakuridhika na uhuru wa nchi yake pekee, alisema: “Uhuru wa Ghana hautakuwa na maana kama nchi zingine za Kiafrika zitaendelea kuwa chini ya Utawala wa Kikoloni”, kuonesha jinsi mwanaharakati huyu alivyokuwa tayari kujitoa mhanga kwa ukombozi wa Bara zima la Afrika.

Hapa ndipo mahala ambapo mama wa Dkt. Kwame Nkurumah, Elizabeth Nyaneba, alikuwa akipika wakati alipopata uchungu kabla ya kumza Kiongozi huyo, eneo hili pia ndilo lilikuwa jiko rasmi la mama huyo akipika chakula kilichomkuza muasisi wa Taifa hili la Ghana. Picha ya Ghana Talk Business.

Mwaka mmoja tu baada ya uhuru wa Ghana, Nkrumah aliitisha Mkutano wa mataifa yote ya Afrika (All African People’s Conference) mjini Accra, Desemba 1958, kuzungumzia agenda ya harakati za uhuru, namna ya kulinda uhuru unaopatikana na kuendeleza mapinduzi ya Kiafrika. Kati ya waliohudhuria, baadhi yao ndio hao waliokuja kuwa viongozi wa nchi zao kufuatia uhuru.

Hao ni pamoja na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Tanganyika); Dakta Hastings Kamuzu Banda (Nyazaland, baadaye kuitwa Malawi); Joshua Nkomo (Southern Rhodesia/Zimbabwe), Dakta Keneth Kaunda (Northern Rhodesia/Zambia) na Patrice Emery Lumumba (Congo Leopoldville/Zaire/DRC).

Wengine walikuwa ni Amilcar Cabral (Portuguese Guinea/Guinea Bissau); Holden Robert (Angola) na Tom Mboya (Kenya) aliyewakilisha Vyama vya Wafanyakazi na ambaye pia alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Mkutano huo.

Muonekano wa Kitanda alichokuwa akilalia Dkt. Nkrumah nyumbani alipozaliwa kijijini cha Nkroful kilichopo Mkoa wa magharibi umbali wa kilomita 83 toka mji wa Takoradi, nchini Ghana, inaarifiwa kuwa pia alikitumia chumba hiki kama maficho wakati alipokuwa rais. Picha ya Ghana Talk Business.

Walihudhuria pia kwa “Mwaliko maalum”, wanaharakati kutoka Zanzibar: Abeid Amani Karume (Afro-Shirazi Party – ASP) na Ali Muhsin (Zanzibar Nationalist Party – ZNP). ASP na ZNP vilikuwa na ugomvi na uhasama mkubwa wa kisera na kimaono kiwango cha kuzuia meli ya uhuru kuong’oa nanga Visiwani.

Wakati ZNP kilichokuwa cha mrengo wa siasa za Kikomunisti na kiharakati zaidi (kwa msukumo wa Abdulrahman Babu kama Katibu Mkuu) kilitaka uhuru mara moja; ASP chenye siasa za kati chini ya Karume kilitaka agenda ya uhuru iahirishwe kwa muda (kauli yake ilikuwa “Uhuru Zuia”) kikihofia ZNP kuchukua nchi.

Karume na Muhsin walipatanishwa na Nkrumah mwenyewe pamoja na Msaidizi wake George Padmore. Wawili hao wakaonywa kuepuka kuwa “Vita vya panzi” enzi hizo za harakati za uhuru. Mapatano hayo, yaliyopewa jina “The Accra Accord” kwa lengo la kuimarisha Umoja wa Kitaifa, ulikuwa “Mwafaka” wa kwanza kwa Siasa za mpasuko Zanzibar, japo haukudumu, ambapo leo uhasama huu umerithiwa na “CCM Zanzibar” na “CUF Zanbar” kwa misingi ile ile ya kale.

Dkt. Kwame Nkurumah akiwa na mama yake Elizabeth Nyaneba. Picha ya AtinkaNews.

Nkrumah alikuwa Mwasisi wa wazo la kuundwa kwa Shirikisho la nchi za Afrika, wazo lililozaa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU, sasa AU). Lengo lilikuwa ni kuona Afrika inajizatiti katika kujenga uchumi huru na imara; kujitegemea na kuunda Jeshi kubwa, imara kuweza kukabiliana na uvamizi kutoka nje na ambalo lingetumika pia kwa harakati za ukombozi wa Afrika.

Ni kwa njia ipi na muundo upi Shirikisho la Afrika lingefikiwa, Nkrumah na Nyerere, majabali wawili wa Siasa za Afrika enzi hizo, walitofautiana. Wakati Nkrumah alitaka Afrika iungane mara moja bila kuchelewa kabla viongozi hawajaanza kunogewa na kulewa madaraka, Nyerere alitaka Muungano wa Afrika uanze kwa awamu na kikanda, kwa nchi chache kuungana kabla ya kufikia Muungano wa Afrika nzima.

Kwenye Mkutano wa Pili wa OAU mjini Cairo, Julai 1964, Nyerere na Nkrumah walishambuliana kwa maneno na ukinzani wa hoja nusura washikane mashati juu ya hilo, ugomvi uliopewa jina “The Great Encounter” (Pambano Kuu) ambapo hoja ya Nyerere ilishinda.

Watoto wakicheza katika sanamu iliyoanguka ya aliyekuwa Rais wa Ghana, Kwame Nkrumah baada ya mapinduzi yaliyoondoa utawala wake Machi 6, 1966. Picha ya Harry Dempster/Express/Getty Images.

Afrika na Dunia nzima bado inajiuliza, ni yupi kati ya wawili hao alikuwa sahihi juu ya kufikia Shirikisho/Umoja wa Afrika, hasa tunaposhudia kwamba hadi leo, Afrika imeshindwa kuungana, huku miungano/jumuiya za Kikanda zikiibuka na kuvunjika haraka na kirahisi? Ni nani huyu, Mwanaharakati Kwame Nkrumah, mwenye kustahili kuitwa “Baba wa Uhuru” barani Afrika; jabali la siasa aliyeweza kusuguana mabega na Mwalimu Nyerere?

Chama cha kwanza cha kiharakati nchini Ghana kilianzishwa mwaka 1947, kikiitwa “The United Gold Coast Convention” (UGCC) chini ya Dakta Joseph Danquah, kilichoanza na hoja ya kubadili jina la nchi kutoka “Gold Coast” kuwa “Ghana” kabla hata ya uhuru.

Kilimwajiri Dakta Nkrumah kama Katibu Mkuu ili kukipa nguvu, kwa kumwita kutoka Marekani na Uingereza alikoishi kwa miaka 12 na kujipatia shahada za juu katika uchumi, Sosholojia na falsafa. Akiwa ng’ambo, Nkrumah alijikita katika kuwaunganisha watu weusi ugenini wajitambue na watambue haki zao na kusaidia uhuru wa Afrika.

Katika vilima vya Karimenga vilivyopo Mkoa wa Kaskazini Mashariki mwa Ghana, kuna nyumba ya ghorofa ya vyumba viwili iliyochakaa na kutelekezwa. Inaaminika kuwa haya yalikuwa ni maficho ya Rais wa Kwanza wa Ghana, Dkt. Kwame Nkrumah. Picha ya GH headlines.

Ni Nkrumah na Weusi wengine wa nchi za Kikarebia, aliyeitisha Mkutano mkuu wa Kwanza wa watu Weusi duniani (Pan-Africanism Conference) mjini Manchester, mwaka 1945 kuzungumzia Mshikamano wa mtu mweusi.

Mwaka 1949, Nkrumah na Danquah walifarakana; Nkrumah akajiengua UGCC na kuanzisha Chama cha siasa za mrengo wa Ki-Karl Marx (Kikomunisti) cha ”Convention People’s Party” (CPP). Mwaka 1951, alishitakiwa na kufungwa miezi sita kwa makosa ya “uchochezi”, akaendelea kupigania uhuru akiwa kifungoni.

Katika uchaguzi wa kwanza mwaka huo, ambapo aligombea akiwa jela, chama chake CPP, kilipata viti 34 kati ya viti 38 vya Baraza la Kutunga Sheria (LEGCO) na GCP cha Danquah kiliambulia viti vinne. Nkrumah mwenyewe katika Jimbo la Accra alipata kura 20,780 kati ya kura 23,122 zilizopigwa; mpinzani wake kutoka GCP alipata kura 2,342.

Nyumba za kifahari za Dkt. Kwame Nkurumah ambazo zimeharibika na kutelekezwa. Picha ya MG

Habari za ushindi huo zilimfikia Nkrumah akiwa jela Februari 12, 1951; naye Gavana wa nchi hiyo, Aden Clarke, akalazimika kumtoa kifungoni siku hiyo na kumwomba aunde Serikali ya Mpito.

Julai 1953, huku akionesha dhahiri kupoteza subira, Nkrumah alishinikiza kuundwa kwa Serikali yenye madaraka kamili “bila kuchelewa”. Hata hivyo, ulizuka mtafaruku kati ya Nkrumah aliyetaka kujenga Taifa huru la kidemokrasia na la kisiasa, na Watawala wa kijadi (Machifu) waliotaka kubakia na madaraka yao ya wakati wa ukoloni, ghasia na machafuko yakazuka na nyumba ya Nkrumah ikashambuliwa kwa mabomu. Kwa kisingizio cha kutaka kupata matakwa sahihi ya wananchi, Serikali iliagiza ufanyike uchaguzi mwingine.

Licha ya ushindi mkubwa kwa mara ya pili kwenye uchaguzi wa mwaka 1954 kuelekea uhuru kamili, Serikali ya Uingereza ilikataa kutamka tarehe ya uhuru na badala yake ikatangaza uchaguzi mwingine kufanyika mwaka 1956. Katika uchaguzi huo, CCP kilipata kura 398,000 dhidi ya kura 299,000 za upinzani; na kwa viti vya LEGCO, kilipata viti 72 kati ya viti 104. Kwa matokeo hayo, Uingereza ikaridhia Ghana kupata uhuru Machi 6, 1957.

Kwame Nkrumah alitabiri mwaka 1961 kitakachotokea leo ikiwa nchi za Afrika hazitaungana kisiasa. Je, nini kitatokea kwa vizazi vijavyo vya Kiafrika ikiwa hatutaiunganisha Afrika leo?

Mwandishi wa Kimarekani, John Gunther aliyekutana na Nkrumah siku ya uhuru anaelezea haiba ya kiongozi huyo katika Kitabu chake “Inside Africa”, ifuatavyo: “Mwendo, mwenendo na hisia (gesture) zake ni zenye mvuto, nguvu na utulivu wa kuhuisha; hana mikogo wala kauli tata za kutia chumvi”.

Nkrumah, akiwa bado kapera hadi Desemba 1957, maisha yake yalitawaliwa na siasa pekee kuliko vitu vingine; hakuwa mpenzi wa michezo, kinywaji, sigara wala starehe za aina yoyote. Alikuwa mtu mpweke, mwenye fikra wa kuwaza na kuwazua nyakati zote na hakuamini wenzake na kwa nadra alitaka ushauri wao.

Aliweza kuchanganyika na wanawake kwa urahisi lakini hakupenda kuhusiana nao kwa karibu, iwe kwa upendeleo maalum wa kivikundi au mmoja mmoja hivi kwamba kabla ya uhuru aliwahi kusema hakuwa na muda wa kuoa, hadi aliposhinikizwa na mfumo wa Serikali baada ya uhuru.

Rais wa kwanza wa Ghana, Dkt. Kwame Nkrumah (kulia), akiteta jambo na Wabunge katika moja ya vikao vya kwanza vya Bunge nchini Ghana. Picha ya Graphic Online.

Bila kumjulisha mtu, lakini kwa shingo upande, na pengine kwa kushauriwa na aliyekuwa Rais wa Misri, Gamal Abdel Nasser; Nkrumah aliamua kuoa mke kutoka Misri; mwanamke ambaye hakuwahi kumsikia wala kukutana naye kabla ya hapo hadi siku alipoletwa Ghana siku ya kufunga ndoa, Desemba 30, 1957, iliyoshuhudiwa na watu wasiozidi 30.

Binti huyo wa Kimisri, Fathia Rizk, aliongea lugha ya Kiarabu pekee, na kidogo sana, Kifaransa kwa kubabia; wakati Nkrumah aliongea Kiingereza kufanya wanandoa hao kuhitaji wakalimani. Kwa nini Nkrumah alichagua ndoa baridi kama hiyo?

Erica Powell, mwanamama wa Kiingereza Msaidizi maalum wa Nkrumah, aliyeachiwa na Wakoloni kumsaidia kuweka sawa mambo ya utumishi na utawala (kama ambavyo tu Mwalimu Nyerere alivyopewa Mama Joan Wickens mwaka 1961) wakati wakiondoka, anamnukuu Nkrumah katika kitabu chake “Private Female Secretary in the Gold Coast”, akimwambia: “Erica, Je, wajua kwamba mimi ni mtu mpweke nisiye na rafiki wala makundi, na kwamba kwangu kilichomhimu ni Kazi tu?”

Aliyekuwa Rais wa Ghana John Dramani Mahama (July, 24 2012 – January 7, 2017). akiangalia sanamu ya Dkt. Kwame Nkuruma iliyopo Bamako, nchini Mali. Picha ya TV3.

Aliwahi kumwambia (1965) pia kwamba, kitu ambacho angependa kufanya ni kujiuzulu Urais na kutumia muda wake wote kwa Umoja wa Afrika. Erica anakiri Nkrumah aliwahi kumtamkia pia kuwa, ikitokea kwamba ameoa, kwake suala la mke, watoto na mambo ya kifamilia kwa ujumla yasingekuwa masuala ya Kiserikali bali ya kibinafsi; akisema “ni hatari sana, na kwa kweli ni ubatili mtupu, kwa mke na familia kujiona kuwa sehemu ya utawala na Serikali”.

Nkrumah alimwambia Erica, ndoa haikumuondolea upweke, akasema: “Wajua Erica; sikutaka kuoa, wala sikuoa kwa kupenda ila kwa sababu ya Urais”. Erica hakuelewa, kwa nini mtu wa hadhi kubwa kama Nkrumah, mwenye elimu, akili na busara kubwa, aliamua kuoa msichana mdogo na ambaye hawakuelewana kwa kizuizi cha lugha. Hapa kulikuwa na mshabihiano uliofichika.

Ilitokea kwamba, Nkrumah alioa Misri si kwa bahati mbaya, kwa Rais mwanaharakati Kanali Nasser, mwenye siasa za mrengo wa Kikomunisti, aliyeingia madarakani kwa kupindua kijeshi Serikali ya Mfalme Farouk mwaka 1956.

Maonesho ya kihistoria ya Dkt. Kwame Nkurumah. Picha ya Brittle Paper.

Nasser na Nkrumah, licha ya kuwa miongoni mwa waasisi wa OAU, walikuwa Waasisi pia wa Umoja wa Nchi zisizofungamana na upande wowote duniani (Non-aligned Movement – NAM), pamoja na Josef Bronz Tito (Yugoslavia) na Pandit Jawaharl Nethru (India).

Wanne hao walikuwa pia wanamstari wa mbele wa kwanza na majabali dhidi ya ukoloni mkongwe, ukoloni mamboleo na ubeberu wa kimataifa.

Lakini pengine sababu kubwa zaidi kwa Nkrumah kumuoa binti huyo wa Kiarabu, ilikuwa ni kujaribu kuimarisha mshikamano wa Kiafrika (Pan-Africanism) kwa kujenga tafsiri mpya kwamba “Mwafrika” maana yake si “Mtu mweusi” pekee, bali ni “mzalendo yeyote mkazi wa Afrika mwenye mapenzi mema kwa Afrika”.

Gari maalum alilokuwa akilitumia Kwame Nkrumah likiwa makumbusho ya Taifa hilo. Picha ya Autojosh.
Muonekano wa Gari maalum alilokuwa akilitumia Kwame Nkrumah. Picha ya Autojosh.

Mafanikio ya Nkrumah kisiasa hayakuwa bila mikwara kama anavyoelezea Genevova Marais, katika kitabu chake “Kwame Nkrumah As I knew Him” kwamba, “Kadri alivyopata mafanikio nchini, ndivyo alivyozidi kutowamini marafiki zake wa karibu, bila kujali jinsi walivyojitahidi kuonesha utii kwake.
Kwa jinsi hii, alipoteza ushirikiano kiserikali na kubakia kuungwa mkono na Wana-CCP pekee, waliomwambia kile tu waliona angefurahi kusikia na kuacha mambo mengine yajiendee hovyo hivyo”. Kwanini?

Erica Powell anasema, tatizo la Nkrumah, na la madikteta wema wote (benevolent dictators) ni kwamba, “alikuwa hatabiriki; kwa haiba, aliweza kubadilika ghafla, akawa mkali kupindukia, asiyeambilika; lakini alikuwa mcheshi pia na mwenye kufikiria upya jambo akiona inafaa kufanya hivyo.”

Nkrumah alipinduliwa na Jeshi lake Februari 24, 1966 akiwa mjini Beijing, China akielekea Hanoi, Vietnam kama Kiongozi wa Kimataifa mwenye jukumu la kusuluhisha vita ya Vietnam, kati ya Vietnam na Marekani enzi hizo za vita baridi. Alirejea Afrika lakini si Ghana, bali kama mkimbizi uhamishoni nchini Guinea.

Moja kati ya nukuu bora alizowahi kuzitoa Kwame Nkrumah.

Mwalimu Nyerere alitaja sababu zenye ukakasi kidogo, juu ya kuangushwa kwa Nkrumah kuwa, “alifanya kosa kuruhusu rushwa na rushwa ikamlemea”. Je, ilikuwa rushwa pekee iliyomwondoa?
Kuanguka kwa Nkrumah hakukuja kwa sababu ya kukithiri kwa rushwa nchini Ghana, la hasha, wala si kwa sababu ya uongozi mbaya au kuharibika kwa uchumi.

Nkrumah aliangushwa kwa kuthubutu kuchokoza ubeberu wa Kimataifa na kwa kutaka kuunganisha Afrika na nchi za dunia ya tatu kupambana na ubeberu huo.

Ndoto ya Nkrumah ya kuunda Shirikisho la Mataifa ya Afrika (United States of Africa) – “USA” mithili ya USA ya Marekani; kuunda ngome ya Kijeshi Afrika, mithili ya Umoja wa Kujihami Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) na kwa kujaribu kuinasua Afrika kutoka kwenye ushawishi wa Mataifa makubwa (Non-alignment) ilichangia pia.

Nkurumah alipenda kutumia misemo mingi ambayo imeacha nukuu mbalimbali zinazoishi hadi leo.

Dalili zilijionesha mapema. Kuchapisha kwake kitabu, “Neo-Colonialism: The Highest stage of Imperialism” (Ukoloni Mamboleo: Hatua ya Juu kabisa ya Ubeberu) Oktoba 1965 kushambulia Ubeberu, kuliitia kichaa Marekani na kufuta msaada wa dola milioni 35 kwa Ghana. Miezi minne baadaye, akapinduliwa kwa msaada wa Shirika la Kijasusi la Marekani (CIA).

Kanali A.A Afrifa aliyeongoza mapinduzi hayo, alielezea sababu hizo miezi mitano baadaye, katika kitabu chake “The Ghana Coup”, kuwa ni “ndoto za Nkrumah juu ya Pan-Africanism na Muungano wa Afrika; kuunga mkono ukombozi wa kitaifa nchini Kongo na kwingineko, na chuki bila sababu dhidi ya nchi rafiki zetu za Kimagharibi.”

Ni ukweli usiopingika, wala si uzushi, kwamba kupinduliwa kwa Nkrumah ulikuwa ushindi kwa ubeberu wa Kimataifa na ukoloni mamboleo Afrika. Kuanzia hapo, msukumo wa Afrika kuungana umetoweka, udikteta na uporaji wa rasimali za Afrika umetia fora, Afrika inazidi kudhoofika katika nyanja zote kuliko mwanzo, haina jeshi la pamoja la kujilinda wala kutetea uhuru wake ila kwa “msaada” kutoka nje. Afrika iko njia panda.

Nyumba ya milele ya Dkt. Kwame Nkrumah.

Dkt. Nkrumah alisoma kwa miaka 12 nje ya nchi na kurudi Gold Coast kupigania uhuru wa Taifa hilo kutoka kwa Waingereza waliokuwa wameishikilia nchi hiyo kama wakoloni na baadaye, alifungwa jela mara kadhaa kwa kusababisha maandamano ya kisiasa, ba hata hivyo, chini ya uongozi wake kama Rais, kulikuwa na miradi mikubwa ya maendeleo katika urefu na upana wa Ghana.

Dkt. Kwame Nkrumah, alizaliwa Septemba 1909 huko Nkroful, Gold Coast (sasa Ghana) – na alifariki Aprili 27, 1972, huko Bucharest, Romania alikokuwa amelazwa kwa matibabu tangu 1971, na anabaki kuwa ndiye kiongozi wa kitaifa wa Ghana aliye mkuu zaidi hadi leo.

Tukutane katika sehemu ya Nne, hapo tutafahamu muangalia Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Simba SC, Young Africans zaiangusha Singida B.S
Rais akiri kutumia kilevi, awataja Polisi