Ni jambo la heri kukumbuka ulipotereza na kufurahia zaidi unaposimama ili usitereze tena. Kwa namna yoyote ile, urafiki ni bora zaidi ya uadui au uhasama hata kama ni mdogo kiasi gani.

Lakini maadui wengi wakubwa ni wale walioanza kuwa marafiki wakashindwa kuusimamia vyema urafiki wao kutokana na sababu mbalimbali.

Wote tunakumbuka kuwa Serikali ya Awamu ya Nne iliyokuwa inaongozwa na Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ilikuwa shupavu na hodari kwenye masuala ya kidiplomasia. Tuliongeza marafiki wengi zaidi duniani huku Dk. Kikwete akiangukiwa na mzunguko wa kuwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuweka jitihada zaidi za kuimarisha Jumuiya hiyo.

Miradi mingi inayokamilika hivi sasa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na barabara na madaraja yanayounganisha nchi hizo, iliasisiwa na juhudi za Dk. Kikwete. Ni heri kuwa Rais John Magufuli anaunga mkono na kuyaendeleza huku akianzisha jitihada zaidi.

Dk Kikwete

Uimara na busara za aina yake za Dk. Jakaya Kikwete katika kushughulikia masuala ya kidiplomasia na ushirikiano wa kimataifa ulidhihirika pale ambapo Tanzania ilipokwaruzana kwa kiasi chake na nchi jirani ya Rwanda ambayo pia ni mwanachama mwenzake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mkwaruzano kati ya Tanzania na Rwanda haukuwa na picha nzuri kwenye Jumuiya hiyo. Suala la Tanzania kuongoza Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Watu wa Kongo kulizima kundi la M23 lilikoreza mkwaruzano huo hasa baada ya majeshi ya Tanzania kueleza kuwa yamewakamata baadhi ya wanajeshi wa Rwanda kati ya waasi nchini Kongo.

Taarifa hizo zilikanushwa vikali na Rais wa Rwanda, Paul Kagame. Pamoja na mambo mengine, Rais wa Rwanda aliingia kwenye msuguano na kutoelewana na Dk. Kikwete.

Vyombo vya habari vilimnukuu Rais Kagame akitoa kauli kali dhidi ya Dk. Kikwete. Japo hakumtaja jina lakini maelezo yake yalitoa picha ya mtu aliyemlenga. Awali Rais Kikwete alisikika akitoa wito kwa Rais Kagame kufanya mazungumzo na waasi wa FDLR.

“Those people [Tanzanian President Jakaya Kikwete] you just heard siding with Interahamwe and FDLR  and urging negotiations… negotiations?  Me, I do not even discuss this topic, because I will just wait for you [Tanzanian President Jakaya Kikwete] at the right place and I will hit you! He[Tanzanian President Jakaya Kikwete]  did not deserve my answer. I did not waste my time answering him…It is well known. There is a line you cannot cross, there is a line, a line that you should never cross. It is impossible…” Kagame anakaririwa na mtandao wa AfroAmerica, alipokuwa akiwahutubia vijana kwenye sherehe za ‘Youth Konnect’, zilizofanyika Julai 30 mwaka 2013.

Kagame

Naye Dk. Kikwete akiwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania, akiongea katika siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, aliwahakikishia watanzania kuwa mipaka yetu iko salama na kwamba hakuna awezaye kuleta ‘fyokofyoko’.

Utakumbuka kuwa hali ilianza kuwa tata kidogo (japo haikuwa rasmi), hasa baada ya Kenya, Uganda na Rwanda kuanza kufanya mikutano huku ikiitenga Tanzania. Hiyo ilikuwa hatua ya kushangaza kwa Jumuiya hiyo ambayo Tanzania ilikuwa na Uenyekiti.

Mgogoro huo pia ulianza kuchochewa na vyombo vya habari vya Tanzania na Rwanda. Rwanda walianza kumvaa Dk. Kikwete kupitia magazeti yao. Walitumia kalamu zao kumpaka tope wakiweka alama ya kuuliza kwenye uraia wake. Hata hivyo, Dk. Kikwete hakukaa kimya, alijibu tuhuma hizo kiutani katika moja ya hotuba zake za kawaida akielezea kuhusu asili yake na mkewe, Mama Salma Kikwete.

Hata hivyo, busara za Dk. Kikwete na uwezo wake mkubwa wa kushughulikia migogoro kati ya nchi ziliwezesha kupooza hali hiyo na hatimaye mambo ‘yalipoa’.

JPM na Kagame

Siku chache baada ya Rais John Magufuli kuanza kuongoza Tanzania, harufu ya uadui kati ya Tanznaia na Rwanda ilipotea ghafla na badala yake, harufu nzuri ya ubani wa urafiki mkubwa kati ya nchi hiyo ulianza kusikika. Wakati huu pia, Rais Magufuli alivaa viatu vya Dk. Kikwete, kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Rais Kagame alianza kuonesha kumkubali sana Rais Magufuli kwa uongozi wake. Wawili hao walikutana na kufanya mazungumzo kwa mara ya kwanza Machi 2 mwaka huu Ikulu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam.

Baada ya kurudi Rwanda, Rais Kagame aliwaambia wananchi wake wazi kuwa atatumia mtindo wa Rais Magufuli katika kubana matumizi nchini kwake.

Siku chache baadae, Ikulu ya Tanzania ilitangaza taarifa ya ziara ya kwanza ya Rais Magufuli ya kikazi nchini Rwanda, ambayo ni safari yake ya kwanza ya nje ya nchi.

Wiki, Rais Magufuli alikuwa nchini Rwanda ambapo alipewa heshima ya urafiki uliotukuka na mwenyeji wake aliyemkabidhi ng’ombe wenye afya.

8

Akiongea na BBC, mmoja wa viongozi wa Rwanda alieleza kuwa katika utamaduni wa nchi hiyo, ni heshima kubwa kumpa rafiki yako ng’ombe. “Unakuwa urafiki uliotukuka, urafiki wa ng’ombe,” alisema kiongozi huyo.

9

Baadae, Rai Kagame alimfanyika hafla kubwa mgeni wake aliyeambatana na mkewe Mama Janeth Magufuli.

Kwa bahati nzuri, wake za marais hao wanaweza pia kuanzisha urafiki mkubwa kutokana na mila na tamaduni za kiafrika, kwa kuwa majina yao yanafanana kwa matamshi. Ni Janeth Magufuli na Jeannette Kagame. Wanaweza kuitana ‘wa jina’ au ‘somo’.

Ni Janeth Kagame na Janeth Magufuli. Ikulu hizi mbili (Ikulu ya Kigali na Ikulu ya Dar es Salaam) kwa sasa wanaweza kuwa na ujirani kama wa nyumba kwa nyumba.

6

Urafiki huo ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi hizo mbili. Bila shaka tutaona ushirikiano mkubwa wa kiuchumi kwani juzi Marais hao walizindua daraja la Rusumo, linalounganisha Tanzania na Rwanda.

Magufuli, Kagame wazindua DarajaDaraja

 

Diamond afuata nyayo za Chidi Benz?
Mbowe aipongeza serikali ya Magufuli