Kufuatia kipigo cha mabao 2-1 ilichokipata Young Africans katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa fainali, Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya USM Alger kutoka nchini Algeria, kiungo mshambuliaji wa timu timu hiyo, Stephane Aziz Ki amefunguka mazito huku akiwaomba msamaha mashabiki na wanachama baada ya kipigo hicho.

Azizi Ki pia katika mchezo huo hakuwa katika kiwango bora na kushuhudiwa akitolewa kipindi cha pili huku nafasi yake ikichukuliwa na Sure Boy.

Aziz Ki amesema kuwa bado wanazo dakika nyingine 90 za kuhakikisha kwa wanapambania ubingwa baada ya kushindwa kupata ushindi wakiwa nyumbani jambo ambalo wanalifanyia kazi kuhakikisha kuwa wanapata matokeo wakiwa ugenini huku akiwaomba mashabiki wa Young Africans kuendelea kuwaunga mkono.

“Tumepoteza mchezo wa nyumbani ni jambo ambalo hatukulitegemea na tunaamini kuwa kama tuliweza kupoteza mchezo ugenini basi na sisi tupambane kuhakikisha kuwa tunashinda mechi yetu ugenini kama wao.

“Mashabiki wanatakiwa waendelee kutuunga mkono katika mchezo wetu, tunafahamu kuwa wameumia, hivyo tunahakikisha kuwa tunaenda kupambana ugenini ili tuweze kuwafurahisha na kurudisha tabasamu kubwa na tufurahi pamoja, kila kitu kinawezekana,” amesema mchezaji huyo

Robertinho auchimba mkwara uongozi Simba SC
MSF yaonya mlipuko wa Kipindupindu, 1120 waathiriwa