Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) imesema inaendelea na uchunguzi wa sakata la Kiungo kutoka visiwani Zanzibar Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’, ili kubaini aliyemshawishi kuvunja mkataba kinyume na utaratibu.

Kamati hiyo tayari imeshatangaza maamuzi ya kumtaka Fei Toto kurejea Young Africans, kufuatia kujiridhisha Mkataba wake na Klabu hiyo bado ni halali na unapaswa kuheshimika.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Said Soud amesema, uchunguzi wao unaegemea kusaka chanzo cha Kiungo huyo kutangaza hadharani kuvunja mkataba wake mwishoni mwa mwaka 2022, huku ikisemekana kuna kikundi cha watu kilimshawishi kufanya hivyo.

Hata hivyo Klabu ya Azam FC inatajwa sana katika sakata hilo, kufuatia kuhusishwa kwenye mpango wa kutaka kumsajili kupitia Dirisha Dogo la Usajili, ambalo rasmi litafungwa Januari 15.

Soud amesema: “Hata hivyo sisi tunasikia kama wewe ulivyosema kuwa Azam FC inahusika katika kumshawishi Feisal ambapo kimsingi ni kosa.”

“Ikibainika Azam FC wamemshawishi Feisal kuvunja mkataba na Young Africans bila kufuata utaratibu, Azam FC tutaifungia”

“Feisal alisimamia kifungu kimoja wakati mkataba huundwa kwa vipengele vingi, unapaswa uvisome vyote kwa pamoja”

“Tulizifungia klabu mbili, Prisons na Singida Big stars kwa makosa ya kuwashawishi Wachezaji wa timu nyingine wakati wakiwa na mikataba wakaomba review…Hata hivyo bado tuliwakuta na hatia TUKAWAFUNGIA”

“Azam ni miongoni mwa vilabu vilizoukuza mpira wa Tanzania ni kujishushia heshima kama wamehusika kwenye hili”

Mgunda amekabidhi kwa heshima kubwa
Said Soud: Wachezaji someni mikataba yenu muielewe