Mdau wa soka nchini Jamal Kisongo ambaye aliwahi kuwa meneja wa kiungo wa klabu ya Simba SC Said Khamis Ndemla, ametoa ya moyoni baada ya kusikia mchezaji huyo amekubali kusaini mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

Imeelezwa kuwa, kiungo Simba SC Said Ndemla ameongezewa mkataba wa miaka miwili wa kuendelea kukipiga kwenye klabu hiyo kwenye msimu ujao baada ya kufikia muafaka mzuri na mabosi wake.

Kisongo ambaye aliwahi kuwa meneja wa nahodha na mshambuliaji wa Taifa Stars Jamal Kisongo amesema kwa hatua aliyofikia Ndemla, anaamini imesababishwa na kuwa na washauri ambao hawamtakii mema katika maisha yake ya soka.

“Ndemla kwa sasa amekuwa na washauri wabaya sana nyuma yake na ndio waliomshauri aongezee mkataba ndani ya Simba SC wakati hapati nafasi ya kucheza hata kidogo”

“Maisha ya soka ni mafupi sana na usipojitambua watu watakusahau kabisa na ndio maana mimi namshauri Ndemla atoke na akatafute Changamoto nje ya Simba sc nadhani mnamkumbuka Ndemla yule aliyetoka Sweden.” Alisema Kisongo.

Awali, kiungo huyo alikuwa anatajwa kutimkia Young Africans ambayo ilikuwa inatajwa kuwania saini yake kwa ajili ya kuiimarisha safu ya kiungo ya timu hiyo.

Chadema yamjibu Lijualikali: "Michango ipo kikatiba, weka akiba ya maneno"
Balozi wa Kenya aomba Corona isiharibu mahusiano na Tanzania