Kiungo wa klabu ya Chelsea Tiemoue Bakayoko amepata ajali ya gari akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake akitokea mazoezini hapo jana.

Ajari hiyo ilitokea muda wa saa tisa mchana karibu na uwanja wa mazoezi wa ‘Cobham training complex’ unaotumiwa na klabu ya Chelsea katika mazoezi lakini taarifa zinaseama Bakayoko hakupata majeraha yoyote makubwa.

Chelsea itakuwa uwanjani wikendi hii katika ligi katika ligi ya Uingereza na bado haijafahamika kana mchezaji huyo atakuwa katika kikosi kitakacho pambana na Stoke City siku ya Jumamosi.

Hii ni mara ya pili kutokea ajali karibu na uwanja huo ambapo mapema mwezi Agosti 25, kijana mwenye miaka 14 aligongwa na gari katika barabara hiyo japo hakuna mchezaji wala kiongozi yeyote kutoka klabu ya Chelsea aliyehusika katika ajali hiyo.

Bakayoko alisajiliwa na Chelsea kwa kiasi cha pauni milioni 40 akitokea Monaco na tayari kocha Antonio Conte ameonyesha imani yake kwa mchezaji huyo kwa kusema ameanza kuzoea mtindo wa uchezaji wa klabu hiyo.

Hapa chini ni picha zinazoonyesha tukio la ajali hiyo na gari aliyokuwa akiendesha bakayoko;

Chelsea midfielder Tiemoue Bakayoko crashed his £150,000 Mercedes SUV on Thursday afternoon

The Mercedes was left submerged in the trees that hang over the road in Surrey before it was recovered

 

 

Video: Serikali yavunja ukimya suala la Tundu Lissu
Makala: Soko la biashara miaka hii ni gumu kulinganisha na miaka ya nyuma.