Mwanahabari na mchambuzi wa mchezo wa kabumbu hapa nchini , Hemed Kivuyo ,Amesema kuwa vilabu vinatakiwa kutokutegemea uzamini wa ligi pekee, bali kutafuta uwekezaji zaidi.
akizungumza na Dar 24 , Kivuyo amesema kuwa suala la uwekezaji kwa vilabu ni mwarobaini wa kiuchumi .
“ushindani utakuwa mkubwa sana isipokuwa baadhi ya timu ambazo hawana uwekezaji na gharama zao ni ndogo kiukweli navyoona wataendelea kusota sana,” amesema Kivuyo .
Kivuyo amesema kuwa pamoja ligikuwa na udhamini vilabu havitakiwi kutegemea pesa hiyo kwakuwa ni ndogo sana kwenye uendeshaji wa klabu, “klabu inapaswa ijitavutie wadhamini na kuachana na ule wa ligi , wajibrand,kitengo chao cha masoko kiwe bora muda wote na wahakikishe wanapata udhamini,”.
vilabu vya soka vinaendelea na maandalizi ya mwisho kuelekea ligi kuu Tanzania bara inayotarajiwa kuanza jumamosi ya Septemba 5 .
Bofya hapa ….