Mkurugenzi wa Mabingwa wa Soka Ujerumani FC Bayern Munich, Hassan Salihamidzic, amesema watafanya mazungumzo na Beki kutoka nchini Ufaransa Benjamin Pavard juu ya mkataba mpya.

Mkataba wa Pavard  FC Bayern Munich unatarajiwa kumaliza mwishoni mwa msimu huu 2022/23, huku akianza kuhusishwa na Mabingwa watarajiwa wa Hispania FC Barcelona sambamba na baadhi ya Klabu za England.

Kwa sasa Pavard amekuwa na kiwango bora tangu atoke kwenye majeraha, kitendo ambacho kimeushawisho Uongozi wa FC Bayern Munich kuandaa mazingira ya kumsainisha mkataba mpya.

Salihamidzic amesema wamejipanga kufanya mazungumzo na beki huyo kwa ajili ya mkataba mpya na malengo ni kuona anasalia klabuni hapo kwa kipindi kingine cha zaidi ya mwaka mmoja.

“Tutazungumza na Benjamin Pavard kwa ajili ya mkataba mpya na tutafahamu kuhusu maamuzi yake yakoje.

“Nina furaha kwa sababu bado yupo na sisi na amekuwa akifanya vizuri, kiwango chake kipo juu, hivyo ninamini mazungumzo yataenda vizuri,” amesema bosi huyo

Pavard alisajiliwa FC Bayern Munich aliyoitumikiwa katika Michezo 107na kufunga mabao manane mwaka 2019 akitokea VfB Stuttgart aliyoitumikia kuanzia mwaka 2016ā€“2019.

Klabu nyingine ambayo Beki huyo amewahi kuitumikia ni Lille ya nchini kwao Ufaransa mwaka 2014ā€“2016, akianza kuichezea timu ya vijana ya klabu hiyo mwaka 2014 hadi 2015.

Mkakati chumba maalum kunusuru ndoa waleta mafanikio
Matic afunguka yanayoendelea Chelsea