Taarifa kutoka nchini Romania katika mji wa Translyvania zinasema miaka ya nyuma kulikuwa na Kanisa lililokuwa na chumba maalum kwa ajili ya kuwafungia kwa muda wa wiki sita wanandoa waliotaka kutengana.

Chumba hicho, ndani yake kulikua na kitanda kimoja kidogo cha kamba, kiti kimoja, meza moja na kabati moja ambavyo vyoye viliandaliwa maalum kwa wawili hao.

Aidha, inaarifiwa pia kulikua na sahani moja, kijiko kimoja na kikombe kimoja ambapo wanandoa iliwapasa kutumia hivyo vitu wote kwa pamoja.

Sasa basi, baada ya miaka mingi kupita taarufa zinasema kulikuwa na talaka moja tu kwani wengi wa waliofungiwa katika chumba hicho walipatana.

Wachezaji Young Africans wapewa nasaha Singida
Kiwango cha Pavard chaishtua FC Bayern Munich