Kocha Mkuu wa Majogoo wa Jiji ‘Liverpool FC’ Jurgen Klopp, amesisitiza kwamba Darwin Nunez anatakiwa akazane kama anataka kuanza kikosi cha kwanza msimu ujao.
Licha ya Mshambuliaji huyo kuonyesha kiwango bora kwenye mechi za Pre Season na kufunga bao dhidi ya Leicester City na baadae kufunga mabao mawili walipocheza dhidi ya Greuther Furth bado anatakiwa aongeze juhudi.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay alianza kwa kusuasua msimu uliopita baada ya kusajiliwa kwa mkwanja mrefu akitokea Benfica sasa matumaini yameanza kuonekana.
Akazungumza baada ya kuifunga Leicester mabao 4-0 juma lililopita Klopp alisema Nunez alionyesha matumani msimu uliopitalakini bado anatakwa akaze sana.
“Nunez anatakiwa pia kukaba kwani ni njia ya mafanikio pia, alinipa matumaini msimu uliopita. Lakini majeraha, kadi nyekundu, mwanzoni hazikumsaidia kabisa.
“Najuwa ubora wa wachezaji kwani Nunez anapokuwa mazoezini anakuwa na kiwango bora sana, kuwa fiti inasaidia sana ngoja tuone baada ya mechi mbili za mwanzo za ligi nini kitatokea.” alisema Klopp
Diogo Jota alifunga bao huko Singapore na makinda wa timu hiyo Bobby Clark na Ben Doak wote walicheka na nyavu.
Juma lililopita Klopp alisisitiza Liverpool inatakuwa kuongeza nguvu kwenye safu ya kiungo kama wanataka kuwa imara msimu ujao baada ya kuboronga.
Liverpool imewapoteza Jordan Henderson na Fabinho
“Muhimu sana kutengeneza kikosi hasa sehemu ya kiungo, tunatakiwa kufanya kitu hapa, tunafanyia kazi na kila mtu anahofia mabadiliko ya kikosi. Hata sisi pia tunazingatia maoni ya mashabiki.” alisema Klopp