Kikosi cha KMC FC kesho kitashuka katika uwanja wa Kaibata mkoani Kagera kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania bara dhidi ya Kagera Sugar utakaoanza saa tatu kamili usiku badala ya saa 16:00 jioni kama ambavyo ratiba ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ilivyokuwa hapo awali.
Kwamujibu wa barua ya TPLB, iliyotumwa Aprili 14 ilieleza kuwa awali mchezo huo ulipangwa kuchezwa saa 16:00 jioni lakini imefanya mabadiliko hayo ya muda kutokana na sababu iliyoelezwa kuwa ni kukamilika kwa miundombinu ya taa uwanjani hapo jambo linaloruhusu michezo ya Ligi kuchezwa usiku.
Kutokana na mabadiliko hayo ya ratiba ya muda, KMC imejiandaa vema na kwamba ipo tayari kwa ajili ya kwenda kuzisaka alama tatu muhimu licha ya kwamba mchezo huo utakuwa na ushindani mkubwa kutokana na Timu ya Kagera kuwa na muendelezo mzuri kwenye michezo yao.
“Safari yetu ilikuwa na nzuri na tumefika salama, tumekuwa na wakati mzuri wakufanya mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo wa kesho, tunafahamu Timu ambayo tunakutana nayo inauwezo lakini KMC inawachezaji wenye uwezo mkubwa na ubora na kwamba mchezo huo upo ndani ya uwezo wetu.
Kwaupande wa Afya za wachezaji , wote wako vizuri , wana morali na hali ya kuhakikisha Timu inapata matokeo kwenye mchezo huo muhimu, na nijambo ambalo linawezekana, kocha Mkuu Thierry Hitimana amefanya maboresho mbalimbali na kwamba kikubwa ni kuzidi kumuomba Mwenyezi Mungu azidi kuwapa afya njema wachezaji wetu.
Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni hadi sasa imecheza michezo 19 na kufikisha jumla ya alama 23 na hivyo kuwa kwenye nafasi ya tisa katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania ambapo mchezo wa mwisho ulikuwa dhidi ya Namungo uliomalizika kwa sare ya kutokufungana katika uwanja wa Uhururu Jijini Dar es Salaam Aprili tatu mwaka huu.
Imetolewa na Christina Mwagala
Afisa Habari na Mawasiliano wa KMC FC.