Kikosi cha wachezaji 24, Benchi la ufundi pamoja na viongozi wa KMC FC wataondoka Jijini Dar es Salaam kesho kuelekea mkoani Kagera kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania Bara dhidi ya Kagera Suger utakaopigwa Jumapili ya Aprili 17 katika uwanja wa Kaitaba mkoani humo.
Mbali na mchezo huo, KMC FC pia itakuwa ugenini dhidi ya Geita Gold FC Aprili 23 mchezo ambao utapigwa katika uwanja wa Nyankumbu ambapo hadi sasa maandalizi vizuri chini ya kocha Mkuu Thierry Hitimana ya kuzisaka alama sita muhimu katika Timu hizo zilizopo kanda ya Ziwa.
Katika mchezo huo dhidi ya Kagera Sugar KMC inaendelea kujiimarisha ikiwa ni mara baada ya kutoka sare ya bila kufungana kwenye mchezo uliopita dhidi ya Namungo ambao ulichezwa katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam Aprili tatu mwaka huu.
Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni imejipanga kwenda kufanya vizuri kwenye michezo hiyo kwa kanda ya Ziwa licha ya kwamba Kagera na Geita ni Timu nzuri na kwamba zimekuwa zikifanya vizuri kwenye michezo yake.
“KMC tunakwenda Kanda ya ziwa kesho, kutafuta alama sita kutoka kwenye Timu ya Kagera Sugar pamoja na Geita, tunafahamu kuwa Timu hizo ni nzuri na zimekuwa na matokeo mazuri kwenye michezo yao, lakini hiyo haituzuii Manispaa ya Kinondoni tukashindwa kupata alama zote kwasababu zipo ndani ya uwezo wetu.
“Tunawachezaji bora na wenye uwezo wakuipa Timu matokeo kwenye mazingira yoyote yale, sikuzote Timu yetu ni imara haijalishi hatujapata matokeo mazuri hivi karibu kwenye michezo mitatu iliyopita, hivyo tunahitaji ushindi kwenye michezo yetu, tunakwenda kwa tahadhari kubwa huku tukimtanguliza mwenyezi Mungu.
Kwaupande wa afya za wachezaji wote ziko vizuri , wanahari na morali , licha ya kuwa tutakuwa ugenini, lakini tunakwenda kuipambania Timu yetu, tunahitaji kuwapa furaha mashabiki zetu, Manispaa yetu ya Kinondoni, na Watanzania wote ambao wanatusapoti, na kikubwa zaidi hatufikirii michezo ambayo ilishapita badala yake tunafokasi kwenye michezo iliyopo mbele yetu.
Imetolewa leo Aprili 12
Na Christina Mwagala
Afisa Habari na Mawasiliano wa KMC FC