Uongozi wa KMC FC umetoa baraka zote kwa kiungo mkabaji wa timu hiyo, Baraka Majogoro aliyeko Afrika Kusini kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika timu ya Chippa United anayoichezea pia Mtanzania mwengine, Abdi Banda.

Nyota huyo wa zamani wa Polisi Tanzania na Mtibwa Sugar yuko Sauzi akiendelea na majaribio huku viongozi wa KMC wakiweka wazi wapo tayari kufanya biashara endapo tu atafuzu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Afisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema wao kama viongozi wanamtakia kila la heri katika safari yake kwani lengo kubwa ni kuona anafuzu.

“Majogoro amebakisha mkataba wa mwaka mmoja ila sisi hatuangalii hilo kwanza kwa sababu malengo yetu kama timu na taifa ni kuona wachezaji wetu wengi wa Kitanzania wanapiga hatua nje ya nchi.”

Banda anayeichezea Chippa alisema endapo nyota huyo atafuzu itakuwa ni faida kubwa kwa nchi kwani itatengeneza timu imara ya taifa, Taifa Stars.

Mkutano Bukombe: CHADEMA imekata pumzi?
Ulimwengu kutambilishwa Singida Day