Kocha wa timu ya Arsenal Freddie Ljungberg amesema kuwa mchezaji wake, Mesut Ozil alikasirika baada ya kufanyiwa mabadiliko kwenye mchezo dhidi ya Manchester City Jana Uwanja wa Emirates dakika ya 59 na kumpisha Emile Smith-Rowe.

Ljungberg amesema Ozil hakupaswa kukasirika kwa kuwa kazi yake ilikuwa ni kutafuta ushindi kwenye mechi hiyo ambayo ilikuwa ngumu kwao baada ya kupoteza kipindi cha kwanza.

Matokeo hayo yanaifanya Arsenal kuwa nafasi ya 9 kwenye msimamo na pointi zake 22 baada ya kucheza mechi 17 huku Manchester City ikiwa nafasi ya tatu na pointi zake 35 na kinara ni Liverpool mwenye pointi 49 wote wamecheza mechi 17.

Kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu England, Arsenal ilipoteza kwa kuchapwa jumla ya mabao 3-0 yaliyofungwa na Kevin De Bruyne aliyefunga mawili dakika ya 2 na 40 huku moja likifungwa na Raheem Sterling dakika ya 15.

TFF yatoa tamko kwenye dirisha la usajili
Serikali kuongeza uzalishaji wa Majongoo bahari