Kocha Mkuu wa CR Belouizdad ya nchini Algeria, Marcos Paqueta amesema kuwa anatarajia kukutana na upinzani mkali kutoka kwa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans katika mchezo wa Mzunguuko wa Kwanza wa Kundi D, Ligi ya Mabingwa Afrika kutokana ubora wa wachezaji wao.
Kauli hiyo ya Kocha huyo kutioka nchini Brazil imekuja kufuatia ubora wa baadhi ya wachezaji wa Young Africans ambao wamekuwa wakionyesha kiwango cha hali ya juu kwa sasa ambao ni Maxi Mpia Nzengeli, Pacome Zouzoua, Aziz Ki ambao kwa pamoja wanaunda utatu wa MAP sambamba na nyota wengine.
CR Belouizdad wanatarajiwa kukutana na Young Africans katika mchezo huo wa Mzunguuko wa Kwanza Ijumaa (Novemba 24) huko nchini Algeria.
Kocha Marcos Paqueta amesema: Natarajia kukutana na upinzani mkali kutoka kwa Young Africans ambayo imekuwa na kikosi kizuri kwa misimu ya hivi karibuni, hivyo lazima tujiandae licha ya kuwa tutakuwa tunacheza mchezo wa nyumbani.
“Young Africans ni timu ambayo imeonekana kufanya vyema hata ugenini kulingana na ya sasa hivyo tunajiandaa kuangaliani namna ganı tutakuwa na wakati bora ili kuweza kupata kilichobora zaidi,” amesema kocha huyo.