Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari imetangaza timu nne zenye wachezaji 22 kila moja kwenye kampeni ya kusaka vipaji kupitia mpira wa miguu katika mashindano yaliyofanyika katika mikoa ya Mwanza, Mbeya, Arusha na Dar es Salaam.

Lengo la mashindano hayo likiwa ni kukuza vipaji ambapo timu hizo zilizochaguliwa zitashinda na kuunda timu moja itakayo julikana kama Safari Champions.

Timu hizo zinatarajiwa kuingia kambini mapema mwezi ujao na baadaye kushindanishwa ambapo wachezaji 22 watachaguliwa ili kuunda timu ya Safari Lager Champions itakayocheza na moja ya timu kubwa katika ligi kuu ya Tanzania.

Makocha Jamhuri Kihwelo na Sekojo Chambua wanasema hili ni zoezi la aina yake na lenye lengo la kuongeza tija katika tasnia ya mpira.

Simba SC yataja sababu kuchelewa kupata kocha
Kocha CR Belouizdad aipa heshima Young Africans