Baada ya kuambulia kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Mtibwa Sugar, Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji FC Masoud Djuma Irambona, amesema ubora wa kikosi cha wapinzani wake ulikua kikwazo kwa timu yake kuibuka na ushindi nyumbani.
Mtibwa Sugar walipata ushindi huo jana Jumapili (April 17) katika Uwanja wa ugenini (Uwanja wa Jamhuri) mjini Dodoma, huku mchezo ukicheza usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Kocha huyo kutoka nchini Burundi amesema Mtibwa Sugar walikua bora sana katika mchezo huo, na hana budi kukubali hilo kutokana na historia ya klabu hiyo ya Mkoani Morogoro kulibeba soka la Tanzania.
“Hakuna asiyejua ubora wa kikosi cha Mtibwa Sugar kwa kuwa tunafahamu Tanzania asilimia kubwa ya wachezaji wazuri kwenye ligi yetu wanatoka mkoani Morogoro”
“Wamecheza vizuri dhidi ya timu yangu, wamestahili kushinda mchezo huu, tunajiapnga kwa mchezo ujao ninaamini tutafanikiwa baada ya kufanya vibaya katika mchezo huu.” Amesema Kocha huyo ambaye aliwahi kuwa Kocha Msaidizi Simba SC.
Ushindi huo umeipeleka Mtibwa Sugar hadi nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kufikisha alama 23, huku Dodoma Jiji FC ikisalia nafasi ya 14 kwa kuwa na alama 21.