Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Mexime anaipigia hesabu kali Young Africans kuelekea mchezo utakaozikitanisha timu hizo katika Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Miamba hiyo imepangwa kukutana Aprili 11 katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam, huku Young Africans ikihitaji kuendeleza ubabe ambao utawawezesha kuusogelea Ubingwa wa msimu huu 2022/23.

Kagera Sugar iliyo nafasi ya saba katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama zake 32, nayo inahitaji kushinda mchezo huo ili kujiondoa katika hali ya kufikirika, kutokana na timu nyingi za Ligi hiyo kuwa kwenye Sintofahamu ya kushuka Daraja hadi sasa.

Kocha Mexime amesema kuwa, kikosi chake kipo vizuri na kinaendelea na maandalizi ya kuikabili Young Africans mnamo Aprill 11, ili kutwaa alama tatu muhimu za mchezo huo watakaocheza wakiwa ugenini jijini Dare salaam.

“Tunaendelea na maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Young Africans, siku zinazidi kusogea na hakuna muda wa kupumzika, tunahitaji kujiandaa vizuri ili kutimiza malengo ya kupata alama tatu za mchezo huo.”

“Ligi ni ngumu na ina ushindani mkubwa hasa katika michezo hii ya mwisho, kila timu inapambana kupata matokeo hivyo tunajipanga kuweza kupata matokeo mazuri,” amesema Mexime.

Mchezo wa Duru la Kwanza uliozikutanisha Kagera Sugar na Young Africans katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mwaka 2022, Wananchi walifanikiwa kuchomoza na ushindi wa 1-0, bao likifungwa na Mshambuliaji kinda Clement Mzize.

Senzo: Ninaiona Young Africans Nusu Fainali
Watatu wakutwa wamefariki wakiwemo watoto mapacha