Baada ya kuupa heshima Mkoa wa Kigoma kwa kuipandisha Ligi Kuu Tanzana Bara Mashujaa FC kwa ushindi wa jumla wa 4-1 dhidi ya Mbeya City, Kocha Abdul Mingange ametamba kuandaa ripoti kabambe itakayoiwezesha timu hiyo kuwa na kikosi imara kuelekea msimu ujao 2023/24.

Mingange ambaye ni Meja Mstaafu wa Jeshi la Wananchi ‘JWTZ’ ametoa tambo hizo baada ya kikosi chake kurejea mjini Kigoma kikitokea mkoani Mbeya, ambako walicheza mchezo wa Mkondo wa Pili wa ‘Play Off’ wa Ligi Daraja la Kwanza (Championship) juzi Jumamosi (Juni 24).

Kocha Mingange amesema anajua sasa wanakwenda kwenye Ligi Kuu ambayo ni ngumu, hivyo inabidi wajipange kwa kila kitu, ikiwemo kuongeza baadhi ya wachezaji wenye viwango na wazoefu.

“Tunashukuru Mungu kwa kupanda daraja, hizi ni juhudi za Mkuu wa Majeshi aliunda kamati ya kuisaidia timu, wachezaji tuliwaongezwa posho, pia mkuu wa mkoa na wa wilaya ambao walihamasisha sana wananchi kuiunga mkono timu na ndiyo maana unaona walijaa sana siku ile pale Lake Tanganyika na hata hapa Mbeya, nusu nzima ya mashabiki walitoka Kigoma, hawa wote wamefanya kazi yangu kuwa nyepesi kidogo,” amesema kocha huyo ambaye aliwahi kuinoa Mbeya City.

Mashujaa FC inaungana na JKT Tanzania na Kitayosce Football Club ambazo zitashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao 2023/24, zikitokea Championship.  

Wananchi: Waziri Mwigulu amekurupuka, hatushirikishwi
Josko Gvardiol anawindwa mitaa ya Manchester