Mbio za Saudi Arabia katika kinyanga’nyiro cha kuwania uwenyeji wa fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2034 zinaweza kuingia dosari kwani Australia imepania kuipiku kwa mujibu wa ripoti.
Rais wa FIFA Gianni Infantino alitoa tarehe ya mwisho ya maombi kwa niaba ya Saudi Arabia na ilipangwa kiwasilisha zabuni hadi Oktoba 31.
Lakini bosi wa Chama cha Soka cha Indonesia (FA), Erick Thohir, ambaye ni waziri wa taifa hilo, ametangaza rasmi wana mpango wa kushirikiana na Australia.
“Tunajadili kuhusu zabuni na Australia, Malaysia na Singapore kwani zilionyesha nia ya kujiunga na sisi.”
Wakati huo huo Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Lokomotiva, Zagreb Dennis Gudasic ni mmoja kati ya wajumbe sita wa bodi ya muungano wa klabu za Ulaya (ECA) uliozinduliwa Aprili kwa ajili ya kushindana lakini alikemea mpango wa kuhusisha klabu katika upigaji kura.
Gudasic ameshutumu ECA na haitaruhusu klabu zote kutoka Ulaya kujiunga na kupiga kura katika mchakato huo na kiongozi huyo alisema kutoka Brussels: “ECA inadai hili jukumu la mataifa yote yenye nguvu, lakini haitaruhusu klabu kupiga kura katika mchakato wa wa kuchagua uwenyeji.”
Juma lililopita kulikuwa na uvumi kwamba uamuzi wa FIFA wa kukabidhi haki za kuandaa Kombe la Dunia la 2030 kwa mataifa sita katika mabara matatu, inamaanisha kuwa michuano ya mwaka 2034 itakuwa ya kuvutia endapo Saudi Arabia itapewa uwenyeji.
Vyanzo vilivyo karibu na Saudi Arabia vimeiambia Gazeti la Mail Sport FIFA ilipanga kuipa uwenyeji taifa hilo mwaka 2034.
Juma lililopita FIFA ilitangaza Ureno, Hispania, Uruguay, Argentina na Paraguay kila mmoja itakuwa wenyeji wa moja ya mechi tatu za ufunguzi katika Kombe la Dunia mwaka 2030.