Gavana wa kijeshi mkoani Kivu Kaskazini mashariki mwa Kongo, Luteni jenerali constant Ndima ametangaza kufunguliwa kwa barabara zinazoelekea katika maeneo yote yanayozalisha kiwango kikubwa cha vyakula mkoani humo.

Maeneo hayo ni pamoja na Masisi, Rutshuru  na maeneo  mengine yanayodhibitiwa na kundi la wapiganaji wa M23.

Akizungumza na waandishi wa habari ,luteni kanali Guillaume Njike msemaji wake gavana wakijeshi ,amedai kuwa hii ni njia pekee ya kuwasaidia maelfu wa raia wanaohangaishwa na vita.

Wakati hatua hii  ya mamlaka yakijeshi imepongezwa na maafisa wa idara za usafiri jimboni humu, maafisa wa asasi za kiraia wameonekana kuwa na mashaka kufuatia mapigano na ukosefu wa usalama kwenye maeneo yalio tajwa  katika tangazo hilo .

Kufunguliwa tena kwa barabara hizi na vijiji vinavyo sambaza chakula  kumetangazwa wakati ambapo mamia ya malori yakubeba mizigo, yalianza kuwasili mjini jana jioni baada ya majuma kadhaa yakiwa yamezuiliwa na waasi wa M23 katika vijiji mbalimbali vinavyo shuhudia machafuko kwa zaidi ya mwezi moja sasa.

Awali, raia wanao ishi katika vijiji, wilayani Rutshuru baadhi  ikiwa ni wale wanao tegemea kilimo,walidai kuingiwa na hofu kufuatia ukosefu wa chakula unaotokana nakuzuiliwa kwao kutoelekea mashambani na kundi hilo la wapiganaji.

Hata hivyo wakaazi wa mji huu wa Goma waliotengwa  na mitaa inayozalisha chakula  kwa sababu ya vita,wamekuwa  pia na hisia tofauti .

Msururu wa magari yenye mizigo kutoka maeneo yanayoshikiliwa na waasi yameendelea kuingia mjini Goma nakushangiliwa na maelfu wa raia.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Machi 3, 2023
Fidia kwa Wafanyakazi: WCF yaboresha huduma kimtandao