KopaFasta Microfinance Limited, imewapatia kadi na mikopo ya riba nafuu wafanyabiashara wa chakula wa soko la Kisutu jijini Dar es Salaam, na kutoa elimu ya mkopo na kufanya marejesho huku ikiwataka kuepuka matapeli wanaotumia jina la KopaFasta kuwatapeli.
Zoezi la utoaji wa elimu hiyo, limeongozwa na Meneja Mtendaji wa KopaFasta Microfince Limited, Patrick Kang’ombe katika eneo hilo na kuongeza kuwa Kampuni hiyo inawagusa wajasiriamali wanaofanya biashara za aina zote, ili kuweza kujikwamua katika kuendeleza biashara zao.
Amesema, “Wajasiriamali tunaowagusa ni wa aina zote mamalishe, wafugaji wa kuku, ng’ombe lakini tunawagusa wafanyabishara wa maduka madogomadogo ambao ni wana kipato kiasi cha kati na wale wenye vizimba ambao wanauza bidhaa kwenye masoko mbalimbali.”
Patrick amesema, Kampuni ya KopaFaster yenye makao makuu yake Barabara ya Garden, Mikocheni Jijini Dar es Salaam, na yenye tawi lake eneo la Tegeta pia inatarajia kuwafikia wananchi wa Mkoa wa Pwani eneo la Kibaha pamoja na Bagamoyo.
Ameongeza kuwa, “Kwasababu mfumo wetu ni wakidigitali kuna baadhi ya wateja wanaofanya kazi kwenye makampuni mbalimbali yenye matawi nje ya mkoa huu hao wanaweza pata huduma hata wakiwa nje ya Dar es Salaam kwasabau tumeshaingia mkataba na waajiri wao na tunaweza kuwapatia huduma wakiwa Arusha, Mwanza, Mbeya na maeneo mengine ya Tanzania.”
Aidha, amefafanua kuwa ili kupata mkopo wa KopaFasta Microfinace Limited, unatakiwa kufikia ofisini na kupata utaratibu wa namna ya kujiunga na KopaFasta na kusema, ”Sisi kama KopaFasta tumejikita katika kutoa elmu katika mitandao ya kijamii kwenye magazeti na njia nyinginezo kuwaelimisha watanzania kwamba huduma zetu ni za uhakika na zinapatikana kwa utaratibu unaofaa.”
“Kwa mfano tukio la leo hapa sokoni limethihirisha kwamba tuko vizuri na baadhi ya wateja ambao tumewapatia mikopo wameshuhudia hilo na wameona utaratibu unavyokwenda kwahiyo niwaombe watanzania na kuwaasa kwamba wasikubali kutapeliwa watupigie namba zetu ambazo tunatoa kwenye matanganzo lakini pia wafike ofisini kupata mikopo,” amezidi kufafanua Patrick.
Amezitaja huduma nyingine za KopaFasta kuwa ni pamoja na mikopo ya tofauti kwa wajasiriamali ikiwemo mkopo wa dhamana ya gari akisema, “Mteja anaweka gari kama dhamana akapatiwa mkopo na akaendelea kufanya marejesho kama kawaida, kuna mkopo wa mafuta ambapo kuna kadi tofauti na ya wajasiriamali, wameingia mkataba na makampuni mbalimbali ya mafuta.”
Nyingine ni “Mkopo kwa watumishi wa umma ambapo mtu yeyote ambaye ni mtumishi wa umma anaweza kuopata mkopo kutoka kopasafasta, ameongeza kuwa pia wanatoa mkopo wa ngao amabo unatolewa kwa makampuni binafsi ya walinzia ambapo mlinzi anawezs kupata mkopo bkabla ya mwishi wa mwezi,” amesema Patrick.
Nao wafanyabishara katika soko hilo, waishukuru KopaFasta kwa kufika na kuwapatatia huduma ya mikopo wakisema itawasaidia kuinua bishara zao na kuongeza kipato, huku wakiwasihi wafanyabishara wengine kutowaamini matapeli na kuwasiliana na Kopafsta moja kwa moja, ili kuweza kupata mkopo wenye uaminifu.