Mmoja kati ya Wanawake wenye uthubutu, Prof. Anna Tibaijuka ameshangazwa na idadi kubwa ya Wanaume katika mjadala wa Kitaifa wa nishati safi ya kupikia, uliozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan hapo jana Novemba Mosi, 2022.

Prof. Tibaijuka ameyasema hayo hii leo Novemba 2, 2022 katika ukumbi wa JNICC uliopo jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa hali hiyo imeonesha matumaini makubwa na kumtaka Waziri wa Nishati, Januari Makamba kutokata tamaa katika kufanikisha lengo lililokusudiwa la matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Profesa Anna Tibaijuka (wa pili kulia walioketi mbele), akiwa katika mjadala wa kitaifa wa nishati safi ya kupikia. Wa kwanza kushoto (walioketi mbele), ni Mama Getrude Mongela.

Amesema, “Inashangaza kuina idadi kubwa ya Wanaume katika mjadala huu ambao unaweza dhani kuwa ni wa Wanawake pekee hili ni jqmbo la kupendeza tuwapigieni makofi kwakweli, ni lazima kuunga mkono juhudi kama hizi bila kujali mfumo wa kijinsia na Waziri nakuomba endelea na mchakato huu utatuokoa.”

Hata hivyo, Tibaijuka amefafanua kuwa kutokana na hali halisi ya Watanzania walio wengi kuwa na kipato cha chini, bado jitihada za kuwaelimisha juu ya umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia unahitajika kwani una manufaa kwa Taifa kwa nyanja mbalimbali za kutoharibu rasilimali za Taifa.

KopaFasta yaleta tabasamu jipya mjini
TFF yasaka mdhamini mpya Kombe la Shirikisho