Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Walace Karia amesema wapo kwenye mazungumzo na kampuni mbalimbali kwa ajili ya udhamini wa Kombe la TFF.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Karia amesema kombe hilo halina mdhamini mkuu na hata kuitwa Kombe la Shirikisho Azam ni kutokana na kutokuwa na mdhamini mwingine.

“Kombe linaitwa Azam kwa sababu tulisaini nao mkataba wa kuonyesha matangazo kwa hiyo hakuna mdhamini mwingine ndio maana,” amesema Karia na kuongeza;

“Akitokea mdhamini mkuu basi jina lake litakaa pale, halafu hata kuitwa hilo jina ambalo linaitwa sasa ni kukosea maana jina lake ni Kombe la TFF.”

Karia amesema wapo kwenye mazungumzo na baadhi ya kampuni kwa ajili ya kudhamini kombe hilo na akipatikan basi mdhamini jina lake litasimama kwenye Kombe rasmi.

Wakati huo huo Shirika la Ndege la Precision Air limesaini mkataba wa udhamini na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuwa msafirishaji rasmi wa Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation CUP), kwa msimu wa 2022/2023, Mkataba huo una thamani ya shilingi milioni 108.

Astaajabia idadi ya Wanaume mjadala Nishati safi ya kupikia
Wallace Karia: Nitakaa pembeni, Mtanikumbuka