Korea Kusini imethibitisha kuwa wenzao wa Korea Kaskazini wameridhia kupeleka wanariadha katika michezo ya Olimpiki majira ya baridi, baada ya pande hizo mbili kukamilisha mazungumzo ya amani yaliyofanyika katika eneo la mpakani.
Msafara wa kwanza wa Korea Kaskazini kuingia Korea Kusini utahusisha wanariadha, maafisa mbalimbali pamoja na waandishi wa habari.
Huu ni mwanzo mzuri wa upatanishi baina ya pande hizo mbili ambazo zimekuwa na mgogoro wa kisiasa kwa muda mrefu.
Ni mwezi mmoja umesalia kabla ya kuanza kwa michezo hiyo ya Olimpiki katika mji wa PyeongChang nchini Korea Kusini na sasa kinachosubiriwa ni endapo Marekani itafuata nyayo za Korea Kaskazini kupeleka wanariadha wake katika mashindano hayo.