Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ameweka wazi kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa alikuwa na kiu kubwa ya kukutana na Rais, Dkt. John Pombe Magufuli toka siku nyingi

Gambo amesema hayo akiwa anaongea na waandishi wa habari na kudai kuwa amefurahishwa kuona kiu hiyo ya Lowassa kukutana na Rais Magufuli imefikiwa jana pale Ikulu na kudai kuwa hata wao kama viongozi wameweza kujifunza jambo kutoka kwa Rais Magufuli kukubali majadiliano na kiongozi huyo wa upinzani.

“Ni kweli kwamba Mhe. Lowassa alikuwa na kiu kubwa ya kukutana na Rais na Mtanzania yoyote mwenye akili timamu lazima awe na kiu hiyo ya kumuona Mhe. Rais kwa sababu yeye ndiye Rais wetu Watanzania, yeye ndiye amepewa dhamana kutuletea maendeleo sisi kama taifa kwa hiyo mtu yoyote hata kama si Mtanzania ana jambo lake lolote la kimaendeleo njia nyepesi ya kulifanikisha ni lazima ampitie mtu ambaye amepewa mamlaka na Watanzania.”amesema Gambo.

Hata hivyo, Januari 9, 2018 kiongozi wa CHADEMA ambaye aligombea nafasi ya Rais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Edward Lowassa alimtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaama na kumpongeza kwa kazi nzuri anazofanya.

Musukuma awavaa Chadema, asema hawana ubavu wa kumfukuza Lowassa
Korea Kaskazini kupeleka wanariadha Korea Kusini