Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku Musukuma amesema kuwa Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema hawana uwezo wa kumfukuza mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho, Edward Lowassa.

Ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na kituo kimoja cha habari ambapo amesema kuwa alichokifanya Lowassa ni kitu cha kawaida kwani yeye ni CCM.

Amesema kuwa hakuna mtu wa kuweza kumfukuza Chadema kwani chama hicho alishakinunua hata Mwenyekiti wake analielewa hilo.

“Chadema hakuna mtu wa kumfukuza Lowassa, Chama alishakinunua na alichokifanya jana kilikuwa ni sahihi kabisa, ingawa hatumtaki arudi CCM,”amesema Musukuma

Serengeti Lite yanogesha ligi ya wanawake,TFF,SBL wasaini mkataba
Gambo afunguka kuhusu Lowassa